Naheshimu Kamati ya Usajili ya Simba SC, ila nauliza Shiboub tuliyemwacha ana tofauti gani na huyu Kanoute tunayemsifu leo?

Naheshimu Kamati ya Usajili ya Simba SC, ila nauliza Shiboub tuliyemwacha ana tofauti gani na huyu Kanoute tunayemsifu leo?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Mtanisamehe kama nitawakwaza ila kwangu Mimi Mightier siiaona tofauti ya Kiungo Shiboub tuliyemwacha kwa sababu za Kipuuzi na leo hii Kumsajili Kiungo Kanoute tunayempamba.

Tena kwa ninavyomjua Shiboub na kumtizama tokea akiwa Kwao Sudan na katika Mashindano mbalimbali ya Kimataifa aliyocheza kwa mtazamo wangu wa Jicho Kali la Kiufundi naona Shiboub amemzidi vingi Kanoute.

Kwa kusema hivi simaanishi kuwa Mightier sijapendezwa na Usajili wa Kiungo Kanoute kwani nimeona ni mzuri ila Simba SC kumuacha Shiboub na kumsajili Kanoute ni sawa na Manchester United FC iachane na Paul Scholes halafu imsajili kwa Mbwembwe Nicky Butt.

Nilisikitika mno Kuachwa kwa Shiboub.
 
Harafu jana mbona sijaona Chikwende akitambulishwa au nae pia alisahaulika?
 
Yule jamaa aliniuma sana kuachwa
Hujanizidi Mimi Ndugu kwani Shiboub alikuwa na Vitu vingi mno kwa Mchezaji wa Kiungo na Kizuri zaidi Kwake pia alikuwa ni Mfungaji mzuri sana tu.

Kilichomuondoa Simba SC ni Kukataa kuendelea kumpa 10% Kiongozi Mmoja wa Simba SC ( namhifadhi ) katika Mshahara wake wa kila Mwezi.
 
sikufurai alipoachwa Shiboub.
Shiboub sio mkabaji ni kama vile tripple C mwamba wa,,,,,,,,,,,

Ila huyu huyu Mtoto kutoka [emoji1159] mwache kama alivo
Nakuhakikishia huyu tutafanya biznes.

Ametumwa kucheza vile na kocha
Na 100% hana deni kwangu.

Wenye deni kwangu ni wale wengine ukimuondoa Sakho.

Nihitimishe
Kile ni kipimo sahihi kabisa kwa timu yetu.

Ila nasikitika kusema wazawa wavivu pale simba wataendelea kusugua benchi

Samahan kwa kutoka nje ya mada
Mana nimejibu na vingine[emoji13]

Kibu Denis kwangu hana deni[emoji122][emoji119]

Wachezaji wengine uwezo wao umeishia pale hapa nazungumzia wachezaji wa zamani.

Nirudi kumuongelea mtoto kutoka Mali, ni mkabaji mzuri sana hasa tunapokuwa hatuna mpira na pia ni mzuri tukiwa tunashambulia
Hana ubinafsi kabisa hakai na mpira kabisa.

Kikubwa jana nime enjoy sana ule mtanange
Mda wote nlikuwa nakodoa macho kwa tv
Ule mda wa kushika simu sikupata kabisa.

Classic game ile
Tp Mazembe wamejiandaa zaidi yetu
Na wameenea kila idara.

Nini kifanyike inabidi fitness iongezeke kwa wachezaji wetu
Mtu yuko na mpira lakin tuko slow.
Tulipoteza mipira mingi dah
[emoji16]
 
Hujanizidi Mimi Ndugu kwani Shiboub alikuwa na Vitu vingi mno kwa Mchezaji wa Kiungo na Kizuri zaidi Kwake pia alikuwa ni Mfungaji mzuri sana tu.

Kilichomuondoa Simba SC ni Kukataa kuendelea kumpa 10% Kiongozi Mmoja wa Simba SC ( namhifadhi ) katika Mshahara wake wa kila Mwezi.
Una faida nae kwani mpaka umuhifadhi
 
kwanza shiboub aliachwa kwa wakati sahihi kipindi hicho ambacho simba namba zote zilikamilika ko kuachwa kwake hakukuwa na kosa na wala hapakuwa na mapungufu baada ya kuondoka kwake

Pili shiboub alikuwa haelewani na kishingo ndo maana aliachwa

Lakini pia dogo yuko vizuri ana mwelekeo mzuri na tutadumu nae kwa muda mrefu kama kiwango chake kitaendelea kuimarika zaidi na zaidi.
 
Mtanisamehe kama nitawakwaza ila kwangu Mimi Mightier siiaona tofauti ya Kiungo Shiboub tuliyemwacha kwa sababu za Kipuuzi na leo hii Kumsajili Kiungo Kanoute tunayempamba...
Umeichangia sh ngapi simba!?
 
Back
Top Bottom