Juzi kati nilikua nimekaa sehem flani mitaa ya sinza ikawa imekuja noah flani ndani ina watu wanne dereva na abiria watatu mmoja kati yao ni demu mkali, mmoja wa wale watu akawa ameshuka akaja tulipokaa alikua anafahamiana na mmoja wa washkaji niliokua nao, tumekaa pale tunapiga stori muda unaenda ila wale wa kwenye gari hawashuki na wako bize na simu, huyu jamaa yangu tuliokua nae akaanza kumzingua yule jamaa aliyekuja na noah "we msenge naona mnazidi kuwapiga tu mang'ombe" yule jamaa akacheka sana akapotezea muda kidogo akarudi kwenye gari wakasepa nikamuuliza yule jamaa yangu hao jamaa ni askari? akanijibu hao ndo wale tuma kwenye namba hii wanapiga hela kinoma pale kwenye gari wanasimu zaidi ya hamsini na wako na connection na watu wa telecoms zote wanaweza kufika hapa wakascan simu zote zilizo ndani ya ya 2km, nilibaki nashangaa tu akaniambia kijana mjini hakuna shamba, na uliwapeleka polisi yeyote ile hawalali