kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,940
- 7,849
Kibaraka Lissu sasa anaipasua CHADEMA baada ya jaribio la mabeberu la kumuweka urais kushindwa vibaya. Kama watanzania wanavyomuelewa Lissu kwamba ni mtu muongo na mzushi sivyo mabwana zake walivyomuelewa. Inaelekea ameweza kuwaaminisha baadhi ya wafadhili wake anaungwa mkono na watanzania ndio wakamwekea yule mwanasheriaAmsterdam kutuletea vitisho vya kijinga.
Kwa wale wafuatiliaji wazuri mambo ya siasa bila shala waligundua wakati Lissu yuko Ubelgiji kabla ya uchaguzi alikua anafanya mambo kama vile ndio rais wa CHADEMA. Ilikua kama kuna CHADEMA mbili maana ilikua vigumu mtu kuamini kama yale anayosema ndio sera ya CHADEMA au yana baraka ya mwenyekiti wa CHADEMA.
Wakati wa kampeni tuliona vile Lissu alikuwa na agenda tofauti na ilani aliyokabidhiwa na CHADEMA. Inaelekea badala ya kuwaambia Watanzania kinachoahidiwa na CHADEMA anasema yale anayoelekezwa na mwanasheria Amsterdam.
Mambo ya kipaumbele kwa maliberali wa Ulaya kwetu Watanzania sio kipaumbele. Uhuru wa mtu kua shoga au malaya kwetu watanzania ina maana gani?
Uhuru wa kuropoka na kupinga kila kitu una maana gani kwetu? Sisi shida yetu kubwa ni maendeleo kiuchumi kwa msingi wa uhuru haki na usawa. Uhuru na haki nchini vipo kiasi cha kutosha wala mtu asitulaghai. Tunachotaka ni maendeleo kiuchumi ya wananchi.
Sasa uchaguzi umeisha Lissu ameshindwa vibaya na kuiponza CHADEMA kushindwa vibaya. Mtu muongo na mzushi anadai magufuli na CCM wameshinda kwa wizi wa kura. Magufuli na CCM wana ufundi wa wizi kiasi gani kuiba kura kwa kiasi hicho bila hata tone la ushahidi wa kufaa mahakamani kupatikana popote nchini.
Lissu badala ya kutaka wagombea wao kukusanya ushahidi wakate rufaa anapokea maelekezo ya Amsterdam wakatae matokeo na kutaka uchaguzi upya vinginevyo eti nchi iwekewe vikwazo tafikiri wao ndio wawekaji wa vikwazo.
Tunachoona sasa ni mvutano kati ya makundi mawili ya CHADEMA. Lile la Lissu linalotaka CHADEMA kususia bunge ili kukidhi matakwa ya kina armsterdam na kina acacia na wale wenye kutaka CHADEMA kutambua na kukubali matokeo ya uchaguzi.
Tuombe mungu kama CHADEMA itapona mpasuko katika hali hii ya kufuata sera za ubinafsi na usaliti kwa Taifa lao.