Nahisi dalili za malaria lakini nimepima Sina malaria

Top gun maverick

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2017
Posts
2,080
Reaction score
2,871
Habari wadau wa jukwaa muhimu Sana kuliko yote maana afya ni mtaji.naenda moja kwa moja kwenye juzi tu nilikuwa nasikia mwili kuuma hasa joints baridi,mwili kuchemka hasa ikabidi niende dispensary kucheki malaria lakini nikaambiwa huna malaria zaidi nikapewa dawa za kutuliza maumivu na dawa za minyoo labda ndo inaweza ikawa sababu ya kukosa hamu ya kula. Lakini hadi sasa Hali inazidi kuwa mbaya zaidi hasa nikisikia tu harufu ya chakula au kuweka tonge mdomoni lazima nihisi kutapika sasa yaani nko dilemma sijui tatizo ni Nini.
 
Kwema.

Pole sana ndugu yangu.

Vipi ulipima kutumia MRDT sio? Kama ndio nakushauri urudie kipimo kwa kutumia B/S.

Pili, je kuna dalili yoyote ya kuharisha? Unahisi maumivu kwenye kiuno/Chini ya mgongo?

Asante na Karibu.
 
 
nenda hospitali kafanye full blood picture mkuu utakuwa na infection, kwa sasa malaria sio ugonjwa tena sijui ni aina ya vipimo au majira yamebadilika maana dalili ni zile zile ila mara nyingi vipimo huonyesha hakuna tatizo
 
nenda hospitali kafanye full blood picture mkuu utakuwa na infection, kwa sasa malaria sio ugonjwa tena sijui ni aina ya vipimo au majira yamebadilika maana dalili ni zile zile ila mara nyingi vipimo huonyesha hakuna tatizo
full blood picture mkuu hapo si ndo Kuna kupima vvu na tangu nizaliwe sijawahi kupima .
 
full blood picture mkuu hapo si ndo Kuna kupima vvu na tangu nizaliwe sijawahi kupima .

hahahah hapana mkuu hakuna uhusiano wowote kati ya kupima VVU na FBP, ila hii inaweza kusaidia jua tatizo lako lakini nahisi yaweza kuwa viral infection mana huwa inadalili kama za malaria mkuu kuwa na amani tu nenda hospital inayoeleweka fanya hicho kipimo
 
sawa sema hio viral infection hatar Sana
 
sawa sema hio viral infection hatar Sana

mkuu kwani viral infection ndo virusi vya ukimwi wala sio mzee kuna virus wa aina nyingi sana hivo ukiambiwa una viral infection haina maana una VVU
 
Mwili kuwa hovyo siyo lazima kuwa ni malaria mkuu,siku hizi watu wengi wamepuuza lishe sahihi na wanakula mavyakula ya sumu tu kama vile chips yai,wali,pilau,sembe,mavyakula ya kukaanga e.t.c sasa unategemea mwili hapo uwe sawa?Kuna uzi hapa JF unaitwa "uzi wa vyakula"kitu kama hicho, sasa kwenye huo uzi watu ni mwendo wa kuposti huko sumu tuuu badala ya vyakula!

Siku hizi badala ya watu kunywa maji kwa wingi wanakunywa soda na bia kwa wingi hata mazoezi rahisi kama vile kutembea kwa miguu hakuna kufanya ni mwendo wa kupanda magari na bodaboda tuuu!!Hakuna kitu ambacho kinaweza kikamuua mtu haraka kama kukosa maarifa/elimu!!
 
Kapime ngoma maana dalili zake km mareria vile
 
hili limenikuta kinamna fulani..
japo mimi nahisi tu joto la mwili kama liko juu hasa nikinywa maji linazidi maradufu & hata ladha ya chakula mdomoni mwangu imebadilika
 
Kumbe unawachoraga tu wanaopost mapochopocho
 
Kumbe unawachoraga tu wanaopost mapochopocho
Rafiki hali zetu ni mbaya sana,kila mtu maarifa hakuna awe ameenda shule au hajeenda wote wako kwenye kuangamia!

Halafu siku hizi watu ambayo wapo kwenye risk kubwa kiafya ni wasomi na watu wenye feza nyingi kwa sababu kundi hili ndiyo vinara wa kutokufanya mazoezi,vinara wa kula nyama za mbuzi kwa bia,vinara wa pombe kali e.t.c ila masikini huko vijijini hali zao ni nzuri zaidi kwa sababu wao ni mwendo wa dona kwa tembere na kutembea masafa marefu huku mzigo ukiwa kichwani!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…