Nahisi Hii ni Faulu Simba Wanataka Kucheza

Nahisi Hii ni Faulu Simba Wanataka Kucheza

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
SIMBA imeamua kukata mzizi wa fitna sasa, imeamua kusajili mshambuliaji wa ‘mauaji’ kutoka nchini Senegal.


Huyo ni Papa Amadou Niang ambaye anatarajia kutua nchini leo Ijumaa akitokea Dakar, Senegal kwa Shirika la Ndege la Kenya kwa ajili ya kumalizana na Msimbazi.



Wakala wa mchezaji huyo kutoka nchini Cameroon, alitarajia kutua nchini jana ili kumalizana na uongozi wa Simba mara mchezaji huyo atakapotua.


[h=1]Taarifa za uhakika kutoka Dakar zinaeleza Simba imeomba ruhusa ya mchezaji huyo afanye mazoezi na wenzake kwa siku tatu, pia imepewa nafasi imtumie katika mechi moja ili kujiridhisha kwa kuwa awali wakala wake huyo Mcameroon, alikataa asifanye majaribio.[/h]
 
[h=1]DATA ZA MSENEGALI WA SIMBA ANAYETUA DAR ES SALAAM LEO, HIZI HAPA...[/h]





SIMBA imeamua kukata mzizi wa fitna sasa, imeamua kusajili mshambuliaji wa ‘mauaji' kutoka nchini Senegal.


Huyo ni Papa Amadou Niang ambaye anatarajia kutua nchini leo Ijumaa akitokea Dakar, Senegal kwa Shirika la Ndege la Kenya kwa ajili ya kumalizana na Msimbazi.



Wakala wa mchezaji huyo kutoka nchini Cameroon, alitarajia kutua nchini jana ili kumalizana na uongozi wa Simba mara mchezaji huyo atakapotua.


Taarifa za uhakika kutoka Dakar zinaeleza Simba imeomba ruhusa ya mchezaji huyo afanye mazoezi na wenzake kwa siku tatu, pia imepewa nafasi imtumie katika mechi moja ili kujiridhisha kwa kuwa awali wakala wake huyo Mcameroon, alikataa asifanye majaribio.

Papa ambaye imeelezwa ni ndugu wa damu wa mshambuliaji nyota wa zamani na nahodha wa Senegal, Mamadou Niang ambaye alikuwa akiisumbua Taifa Stars kila walipokutana nayo, anaelezwa kuwa mmoja wa washambuliaji wenye kasi.


Taarifa za uhakika zinaeleza Niang atawasili nchini saa 3:10 asubuhi akitokea Dakar baada ya kupitia katika miji miwili ya Abidjan, Ivory Coast na Nairobi, Kenya.


Safari yake kufika Nairobi kutoka Dakar itakuwa ya saa 10 na dakika 40 na saa 1 na dakika 25 kutoka Nairobi hadi Dar es Salaam. Maana yake atatumia saa 12 na dakika 5, kuifuata Simba ya Dar es Salaam ambayo imemwambia ‘njoo tuone'.


Moja ya sifa zake kubwa ni kuwatoka mabeki, lakini ana uwezo wa kupiga mashuti makali kwa miguu yote.


Simba imeamua kujiridhisha na sifa hizo kwa siku ilizopewa ikiwa ni pamoja na kumtumia katika mechi moja ya kirafiki halafu itachukua uamuzi kama inambakiza Dar es Salaam au arejee kwao Dakar.
 
Hivi dirisha la usajiri si limefungwa Jana saa sita usiku
 
nimefarijika kwamba kumbe baada ya dirisha kufungwa timu zinweza kuongeza mchezji wa kigeni lakini watatozwa faini ya shilingi laki tano
 
Karibu sana Msimbazi, Papaaa Niang.

karibu sana pápa niagi ligi kuu bongo,,vpl ila Uwe makin huku figisufigisu nyingi na misumari(ndumba) nje nje yasije yakakukuta ya Dán Serunkuma....:.........
 
Copy & paste is the way to go. If Young Africans SC sign a white player,we will also do the same.
 
amavubi..naomba walau historia ya mchezaji huyo uliemsifia..vilabu alivyochezea..maana yake kizur chajiuza
 
Back
Top Bottom