May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Huyu Jamaa yangu kutoka Arusha yupo Dar kwa wiki kadhaa sasa. Siku kadhaa zilizopita akiwa anaangalia mpira kwenye kibanda umiza ile mechi ya Yanga na Kengold, kipindi cha pili mwishoni alianza kujisikia kizunguzungu kikali,anasema macho yake yakawa yanashindwa kuangalia screen, kichefuchefu na jasho linamtoka sana, akaomba asaidiwe atoke nje, akaenda akajilaza barazani kwa muda mpaka alipojisikia vizuri, akaondoka kwenda kwake.
Siku kadhaa tena baadae akiwa kwake usiku hali ile ilimrudia tena, akahangaika mpaka akalala asubuhi hali ikawa mbaya zaidi akakimbizwa Zahanati ya jirani. Akachukuliwa vipimo ikaonekana presha ,sukari, maleria, wingi wa damu vyote vipo sawa, ila bado Mgonjwa yupo hoi.
Akawa refered Kimara Health center, Kimara wakarudia vipimo vilevile nao hakuna walichogundua. Kuna dawa wakamchoma na kumtaka arudi nyumbani ingawa bado hali yake ilikuwa haijatengemaa na walikuwa wanasisitiza kuwa hawaoni tatizo hivyo hana sababu ya kuendelea kuwa pale,jambo lililomshangaza sana Mgonjwa.
Swali ni je huyu hakuhitaji tiba ya heat stroke kwa dalili zile badala ya Watabibu kuridhika tu kuwa hawaoni tatizo kwenye vipimo vyao? Nini tiba ya heat stroke na je haiwezi kumshambulia tena.