Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.

Usichoke wala usisikitike kipindi kigumu kama icho ila kumbuka ibada sana.jaribu kutafuta hata mikoani kwenye makampuni ajira sio mjini tu
 
Nafikiri pia inategemeana na misingi mliojijengea maana sisi bwana we huwa tunasamehe ila hatusahau. Tunasubirigi siku ulivuruge ndio hapo paap tunakukamatia, labda mtu awe na busara za hali ya juu sana.

I have a friend nae mume wake aliwahi kupitia hali kama hii, ila kutokana na kwamba her husband was always good to her alichukua nafasi yake alisimama na mume wake na akamchukulia mkopo ambao aliutumia vizuri na leo wamesimama kabisa. Lakini kabla ya hapo walikaa chini wakazungumza wakapanga mipango inayotekelezeka na wakawa wana na options kabisa.

Masualaa ya biashara hayahitaji kukurupuka, lasivyo ndio mtu ataona bora akabeti au apeleke kwa matapeli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesoma vizuri alimsaidia mke wake mtaji wa Milioni 6 ili akaanzishe biashara, hiyo haitoshi kuonesha wazi kwamba alimjali mke wake na alipenda kuona nae ananyanyuka kuongeza kipato cha familia pamoja na mahitaji yake binafsi?
Chakii sidhani kama umenielewa hapo niliposema muwatende mema. Kumpa mtu mtaji wa biashara pekee haitoshi. Sisi ni watu wa hisia zaidi. Wanaume mnaposhika pesa huwa mnajisahau sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeusoma huu uzi nimemkumbuka mke wangu kipindi sina shughuli tumepunguzwa kazini. Mungu ni mwema alinishika mkono pamoja na mashinikizo mengi sana kutoka kwa ndugu zake

Hongera sana kwa kuchagua vizuri ndugu! yawezekana ukaishi mda mrefu sana maaana hawa wengine acha nsiongee sana
 
Mkuu usikate tamaa na kufikiria kujidhuru. Hiyo ni miongoni mwa mitihani ktk maisha ya ndoa. Tupo wengi ambao tunapitia vipindi kama hivyo ila ni kwa imani tu ndipo tunapoweza kushinda.
Maadamu watoto wanalala na kula hata kama ni kwa wakwe we pambana popote ukipata mwisho utaungana nao tena.
 
Pole kwa yaliyokukuta, but mimi nimesikitishwa zaidi na tabia ya mkeo kuliko hata matatizo yaliyokukuta. Haiwezekani kipindi hiki kigumu anakuonyesha reaction ya namna hiyo. Unless ndoa yenu ilikuwa na migogoro au maybe ulikuwa unamnyanyasa, kipindi hiki mkeo ndiyo alipaswa kuwa msaada mkubwa sana kwako kisaikolojia kuliko kipindi kingine.
 
Kama hii simuliizi ni ya kweli Kwanza kabisa pole na matatizo yalokupata
Mkeo hakufai kabisa kwanin akukimbie kwenye matatizo ?na baba wa watoto watatu kabisa hata kama mngekuwa hamjazaa hakupaswa wala kuthubutu ,anakupenda ukiwa na pesa tu pili kapata kibarua alitakiwa akubebe akulee akutunze kwa kidogo anachopata hadi hapo utakapopata kazi ,kama ni kweli kafanya hivyo hakufai maisha yako yote Mungu anakupa funzo na kukufunua macho uone
Matatizo ni sehemu ya maisha mlilie muumba wako akupitishe kwa haya magumu unayopitia
Pia inatufundisha tusitegemee chanzo kimoja cha pesa tuwe ma vyanzo vingi vingi vya kupata pesa
Nakuombea kila la kheri urudie hali yako ya zamani

Wanawake tubadilike pia jamani tusiwakimbie waume zetu kisa pesa tuishi katika hali yoyotw ile tukiwa pamoja na kubebana


Jaman wenye uwezo wa kutoa ajira toeni kwa huyu kijana
 
kwanini usitumie elimu yako kujiajiri?

kwa kuwa mil. 6 ambayo ulimpa mkeo kwa ajili ya biashara ikateketea(siyo msimamizi mzuri wa biashara)hivyo uza tena hiyo gari ulionayo ili upate mtaji wa kuanzisha biashara yako kwa kuisimamia mwenyewe.
 
Pole sana kaka, hakika utanyanyuka...

Ila ulifanya makosa sana kumiliki magari matatu wakati unakaa nyumba ya kupanga. Huyo mkeo pia mwangalie kwa makini, yawezekana ndio wale wanawake wa mjini wanaopenda maisha ya anasa..

Pole sana, Maisha ni mapambano usikate tamaa na huu ndio wakati sahihi wa kuwajua marafiki zako wa kweli..
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…