Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.
Acha kabisa kuwaza ujinga kama huu. Kuna watu wapo Muhimbili ICU wanapigania maisha ila wewe unawaza kujiua tena bado unamiliki gari ndogo ya kutembelea?

Mandela alikaa jela miaka 27 akaja kutoka akawa Rais wa Afrika ya Kusini.
 
Pole mkuu
Changamoto Katika maisha ni kawaida na ipo siku zitaisha.
Bado unayo nafasi,haijalishi umeanguka na kufeli Mara ngapi amini unayo nafasi ya kufanikiwa tena.

MUNGU anakupenda na Ndiyo maana amekupa nafasi ujaribu.
Kujiua siyo jibu la matatizo yako,
Kukata tamaa hakuwezi badili chochote kwako.
Amini Mungu ni mwaminifu Katika nyakati zote,amini atadhihirisha uaminifu wake kwako.
Usichoke kupambana,jipe moyo mkuu
Utashinda.

Mshukuru Mungu kwa yote,kuna watu wanatamani hata wangeipata hiyo afya..wapo vitandani hawawezi kunyanyuka.
Lakini wewe MUNGU amekupa hicho kibali.

Nakutamkia ushindi,
Sina hela wala ajira ya kukupa ila amini haya maombi ninayokuombea Mungu atakuvusha..Amin.
 
Ukweli, hii ndio namna sahihi ya mtu (member) anavyo takiwa kufanya pindi anapo kwama.
Sio Jambo jema na wengi tunakosea sana tunapokuja na ID mpya pindi tunapo kwama.
Member anapokuja na ID yake ilio zoeleke, inawapa wengine nafasi ya kumsaidia kwakua walau wengi wanakua na ufahamu kidogo kuhusu muhusika.
 

Oooh jamen mpeni connection msiishie kutoa pole tu
 
Ila pia sio wanawake tu hata wanaume huwakimbia wanawake na kuwaacha walee watoto peke yao tena kwenye umaskini mkubwaa


Jaman kama tunaweza mmoja ajitolee kuhakikisha kama ni kweli tumchangie hata kidogo tulichonacho wenye uwezo wa kutoa ajira saidieni msiishie tu kutoa maneno tunaweza fanya kitu kikamsaidia
 
pole sana mkuu,Mungu yupo na anaina yoote hayo usijali sana yatapita
 
Pole sana
cha kukushauri kubali hilo swala kwamba umefilisika na unaanza moja.
Utapata amani fulani /Halafu focus na maisha yajayo usichague kazi /kichwani kwako iwepo ile kauli ya wahenga kuwa ukupigao ndio ukufunzao.

Shukuru hata umewahi kuwa na maisha hayo maana kuna watu wamezaliwa kwa ugwadu wanaishi kwa uchungu sikuzote.
Utakaa sawa soon sa sijui utamrudisha mkeo?
Mshukuru Mungu kwa kila jambo - Move on
 
Kama Kuna wanna Jamii forum wanaoishi Bunju tunawaomba mfuatilie huu mkasa kwa Hali na Mali ili kupata uhakika ili watu wawe na amani na msaada watakaoutoa.
 
Ila wewe naye unamapungufu yako yaliyomuweka mkeo mbali na wewe Sasa kutumiana msg na housegirl za nini? Tena mshahara analipwa na mkeo, kuhusu kuumwa pole sana na hayo masaibu ya kukosa kazi mwenye connection akusaidie Ila ukishapata kazi jitahidi ufungue biashara ndogo utakayoweza kuisimamia mwenyewe, pia kuendelea kukaa kwa watu siyo vizuri Kama mambo hayaeleweki jipe wiki then urudi kwenu kwa vile wazazi wapo nirahisi kujipanga ukiwa chini yao.
 
Pole mdau kiufupi kushuka kimaisha Ni Jambo la kawaida,Ila kikubwa tu maradhi uliyonayo ndo mtihani ulionao ,Cha pili mkeo ndo anazidisha maisha yko yanakua magumu ,kushuka kimaisha ndo mnatengana au ndo uliamua ,inabidi ukubali kwamba umeshuka na uanze kuishi maisha ya chini kabisa ilitakiwa upange vyumba viwili uswahilini ambayo jumla ingekua 50000 ,pia ungeuza hio gari ndogo uanze biashara ,hata wazo la biashara Niko tayari kukusaidia ,Mimi yalinikuta niliposhuka kimaisha nami nilikuali kuanza chini ,lakini kuhusu kuomba kazi utasubili sana kipindi Ni kigumu hiki kazi hamna, na mkeo asikichanganye mwambie mkapange uswazi na Pato lake liwe la familia kabisa nawe ,hakikisha mkeo unammiliki usimuogope
 
pole sana mkuu mungu akutie nguvu haupo peke yako unaepitia hali hii
 
POINT: Huyu tumchangie nauli ya Mwanza akajipange kwa wazazi wake kuliko kuwa mzigo kwa marafiki
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…