Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Kaka pole mno ...Ushindi wako ukaribu mno..huna haja ya kukata tamaa...ninaamin Mungu ana jambo jema kwako usipokata tamaa...nimepitia haya pia mpaka leo sina ndoa japo nimerudi na maisha mazuri sio kama xaman nilijifunza kutokata tamaa...inapotokea chochote juu ya kazi tutashtuana basing on your experience
 
Pole sana Mkuu. Mungu ni mwema, mwamini yeye nausikate tamaa kabisa. Ili andiko hakika litakupa relief nautakutana na watu wenye msaada humu humu. Kikubwa endelea kupambana na hakika bight future is yours, just the matter of time.

Pamoja Mkuu[emoji1488][emoji1488]
 
Pole ndugu.
 
Hebu ondoa ufeminist wako hapa, mwanamke mpumbavu wew, jamaa ameleta mada anataka msaada km huna msaada kanye ulale, jinga moja
 
Brother

Pole sana aisee, Kwenye maisha tunapitia changamoto nyingi.

One Question: Kwani ukweni uliwakosea nini mpaka unashindwa kujisalimisha? Naona kuna tatizo somewhere. Kuna familia wakwe ndo wanawatoa wana, kwanini wewe uogope kwenda?

Second Qn: Kama ukweni hakuna neno, mkeo bado hakuthamini basi haukua na mke bali ni msaka mali na vitu vidogo vidogo.

Advise: If all other factors remain constant naomba upambane urudi tena kwenye fomu lakini usifikirie kurudiana na mkeo tena sababu hastaili kuishi tena na wewe. Anapata visenti lakini bado amekutupa.

Kuna somo la kujifunza sio tuwe na ajira na tunaishi maisha ya kifahari halafu hatuna alternative sources of income, tutakuja kuchekesha watu mwisho wa siku na tutawapa nafasi wabaya wetu ya kutunanga.

Brother keep on fighting hata kama kuna laana umepata na huwezi sema why, pray ask for forgiveness na nina amini utanyanyuka tena. Hakuna dhambi ama laana/curse inayodumu milele. Rudi kundini halafu God will pave the way na utapata kazi nyingine ama utapewa mbinu za biashara.
 
Kwanini asitumie hiyo gari kutengeneza kipato ?
 
Kwanini asitumie hiyo gari kutengeneza kipato ?
Myulize mwenyewe akujibu
Unajua mtu akizoea maisha ya raha basi ikija shida kidogo tu Analia weee

Hapo kwa cheo chake kazini na maisha ukute hata kuendesha uber anaona aibu
Kuhamisha watoto shule za ada ya kawaida anaona aibu
Kuhamia nyumba yake ikiwa haijaisha hawezi
Kula kwa mama ntilie ubwabwa na maharage anaona aibu..
Anakata tamaa ilhali ana gari,nyumba
Wakati kuna msukuma guta kariakoo ana mke Na watoto wanaishi tandale na haijui million moja,gari wala kiwanja but anafight

Mimi nna matatizo zaidi ya huyu kaka mtoa mada but still sikati tamaa
 
Nimeongea nawew personally, unajua mnaidharau sana depression, lakin huu ni ugonjwa mkubwa sana, na aggravating/relieving factors zake kubwa ni maneno pamoja na uwepo wa dawa lakin maneno yana play role kubwa, mtakuja msababishe watu wajinyonge.
Soma tena ujumbe wangu, this is a social platform. Ni ujumbe kwa kila mtu, kama wewe haukufai yupo unaemfaa.

Wanaume mkishika pesa msijisahau tu, kuna kesho na mkeo ndio aweza kuwa msaada wako mkubwa au akakuzidishia depression kulingana na ulivyokuwa unamtreat.

BTW wewe ulivyonitukana ndio umenisaidia? Au hapo hujatumia maneno umetumia maji eeh!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeisoma story yake inasikitisha na kushangaza.

Alikosa kazi akaamua kuuza gari ya kwanza apate hela za kumpa wife afanye biashara akazila.


Akauza tena gari ya pili kwajili ya kupata pesa ya matumizi na ada !!!!!.

Bado ana gari nyingine lakini analia njaa ???

Huku ni kukufuru Mungu tu kuna wenzetu hawajawahi kuitwa hata interview, hawana baiskeli wala bodaboda lakini wanaishi na hawajawahi kukata tamaa.
 
Mkuu mimi niliwahi kupoteza kazi katika mazingira kama hayo mbaya zaidi ndio ilikuwa kipindi namchumbia mke wangu.Nakuelewa unachomaanisha Sasa naomba nikuunganishe na jamaa zangu Fulani hope watakusaidia ila naomba tusifahamiane na hata ukifanikiwa usinitafute tujuane pili nitumie namba yako ya mpesa au tigo pesa inbox Mimi nitafanya muamala kea wakala tu pole sana mkuu // Soma kitabu cha ayubu ukumbuke mapito aliyopitia na jinsi Mungu alivyomuinua Tena baadae.

Superbug.
 
Toka nizaliwe leo ndiyo nimeona mtu aliyekata tamaa ya maisha huku anamiliki gari [emoji2297][emoji2297][emoji2297]
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…