Nahisi kama nimerogwa

Ni kweli unalogwa na anaekuloga ni yule ambae anajidai kila siku anataka kujua unaendeleaje anafanya hivyo makusudi ili ajue maendeleo yako na akiona una nafuu anaenda kukupiga spana zingine, hii yote inatokana na tabia yako ya kueleza watu mafanikio yako au malengo yako mazuri uliyo nayo.

Binadam ili ufanikiwe ni lazima uwe na Siri na ndo maana hata serekali inatunza sana Siri zake, haifai kueleza watu malengo yako mazuri uliyo nayo yafaa tu waone tayari ulisha fanikisha lengo lako ila ukiwaeleza mapema n lazma watakutengenezea fitna, matatizo ili ukwame usifikie malengo yako au usiyafurahie mafanikio yako uliyo yaweka wazi mbele yao.

Kila nikikuangalia naona una hali mbaya sana leta kuku, mchele, nazi na mafuta ya alizet na Tsh 20k kwa ajili ya sadaka ya wazee ili tukubitu

Zingatia: usiwahi kumuamini mtu yoyote hata Mimi usiniamin yachukue yanayo faa yatakusaidia na yasiyo faa achana nayo kwakua kila binadam ameumbwa na akili.
 
Ukilala,ukiamka muombe na mshukuru Mungu.
Fanya ibada na kuwa mtulivu.
Fanya mazoezi.
Kunywa maji meengi.
Jaribu kuwa unajimix na watu kidogo.
Kama unaishi mitaa yenye nafasi nafuta baiskeli, jioni na siku za weekend uwe unaendesha...
Mwisho na muhimu sana, jaribu kukubaliana na kumaintain ulichonacho, fanya unachoweza usichoweza acha jipe muda, kuwa busy usiku na mchana..
 
Chemsha maji usiku weka kwenye chupa!asubuhi ukiamka chukua kikombe kikubwa cha nusu lita weka maji moto nusu au zaidi halafu changanya na ya Baridi yawe vugu vugu!kunywa kikombe kimoja kikubwa vugu vugu asubuhi na jioni!!!uje utupe mrejesho jamvini!!!
 
Kwisha

Kwa nini umechagua ili jina, kuna nguvu iliyokufanya kuchagua ili jina

Magonjwa mengi uliyoyaeleza hapo juu chanzo chake kikubwa ni
Hofu, Wasiwasi, mashaka
Kama utafanikiwa kushinda hivyo vitu hayo maginjwa na matatizo yako yataondoka

Nasikitaka kuona matatizo yako umepeleka moja kwa moja kwenye Uchawi, hofu ya uchawi itakuandama sana

Tiba yake ni Yesu
 
Hujarogwa wewe... Huenda unakaa sana kwenye kiti , halafu hunywi maji kwa wingi... Jitahidi kunywa maji kwa sana na fanya mazoezi
 
Hapo huna tatizo lolote zaidi ya hofu(anxiety) ni mbaya sana...Mimi kuna kipindi nilikuwa nahisi nakufa hivi yaani mara miguu iwake moto mara mkono uume mara kichwa kiume yaani full shida...Chakufanya fanya zoezi karibia kila siku,punguza vyakula vya mafuta,vyakula vyenye sukari ya kuongeza pia acha,kama unatumia soda esp coca au pepsi acha kabisa..Lastly uwe unapenda kula kitu kinaitwa almonds then njoo utupe mrejesho
 
Nisaidie bro tatizo la tumbo kujaa gesi au chakula kutosagwa vizur ulitumia dawa gan kuondoa Hilo tatizo maana na mm Hilo tatizo huwa linanisumbua sana
 
Unapata ajira unaanza kututukana mtaani ukipita husalimii watu wakati kipindi kile hadi sigara unagongea maskini wacha ukomeshwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…