Nahisi maisha yamenipiga vibaya mno hadi naona aibu

Ameen, barikiwa sana [emoji120]
 

10 years to come utakuwa na miaka 35, bado kijana kabisa, weka tu malengo yako ya miaka mitano hadi 10, achana na hao waioooa, unaweza kuoa hata ukiwa na 40s kama kina Zito kabwe.

You still have time Mkuu. Kikubwa uzima.
 
Mkuu[emoji23][emoji23]eti mngenikuta Mirembe nimejikuta nacheka tu
 
Nimemaliza olevel 2014 Kama wewe na Nina miaka 25 kama wewe ila niamini mimi hujachelewa chochote bro usikate tamaa huu ni umri wetu wa kupambana kutimiza malengo yoyote tuliyoweka haijalishi yatakamilika lini maana duniani hakuna anae wahi Wala anaechelewa kila kitu kinakuja kwa wakat wake na siyo muda wa kukata tamaa

Kufikiria yaliyopita na kutamani usivyo navyo vitakufanya ushindwe kufurahia neema uliyo nayo sasa, acha kutaman maisha ya wengine maana Kuna watu wanayatamani maisha yako pia
 
Achana na Diploma kaoe na Wewe ndugu. Maisha Hayana Fomula ukiangalia Ya Watu Ukaacha Kufanya Yako Utaanguka Pabaya sana
 
to me at @ 25 you still have a lot to do, still young and nothing to worry about !!
 
We dogo tema mate chini. Nyie watoto wa juzi mmeharibiwa na hizi social networks. Haya makitu ilibidi kwa sisi weusi yasifike maana yameleta athari hasi kuliko chanya.

Umri wako huo sio wa kuongea hayo, watu mpaka 29 ilikua bado ni ungaunga. Tena una nafuu una back up ya kaka wa damu.
 
Watoto wa cku hizi mna haraka sn ya maisha, kipindi kile 25 mtu ndiyo alikuwa anaingia form5 na akaja kuwa boss mkubwa tu.
Kabisa aisee back in days. Sijui siku hizi kwanza ni nini imekua, form 1 unakuta ni katoto kadogo unadhani labda ni mwanafunzi wa darasa la 2.

Ukiuliza unaambiwa form 1 nabaki nashangaa.
 

Mimi kaka yako nilitoka kwa mlezi nikiwa na umri wa miaka 28! Wewe na miaka 25 unapagawa?

Muhimu ujitahidi tu kumheshimu na kumnyenyekea shemeji yako.

Yaani ikiwezekana mlambe mpaka miguu!

Maana ukimzingua tu, basi umekwisha.
 
Unaambiwa ingekua inawezekana shimo lichimbwe alaf kila mtu aende akamwage matatizo yake pale, baada ya kuyaona ya wengine kila mtu angeingia kuyaokota ya kwake na kuyakumbatia.
Ni kweli yaani ukipata kujua mazito wanayopitia wengine utajiona yako ni chamtoto.

Kuna kipindi nilipokuwa chuoni katika Ile kipiga stori wenzangu walikuwa wakinieleza matatizo yao, asee nilijiona kumbe sina matatizo ya kutisha, yaani kuna watu wana matatizo we acha tu.
 
Unaambiwa ingekua inawezekana shimo lichimbwe alaf kila mtu aende akamwage matatizo yake pale, baada ya kuyaona ya wengine kila mtu angeingia kuyaokota ya kwake na kuyakumbatia.
Dah basi mzee [emoji22]
 
[emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…