Mpaka sasa nina miaka 25 ndio kwanza nipo Diploma mwaka wa kwanza Semester ya 2 inaanza tarehe 4 Aprili 2022. Bado nakaa na kaka yangu japo naye ana familia yake.
Najihisi kama nimechelewa kuanza maisha vile, nimesoma kwa kuungaunga tu, washkaji na rafiki zangu niliomaliza nao sekondari mwaka 2014 wengi wao wameoa, wengine washaolewa.
Yaani nikionana nao au kupishana nao njiani ni aibu tu, bora tuishie kuchati tu kupitia aidha sms, WhatsApp, Facebook.[emoji2960] Nipo tu kama digidigi vile sina hili wala lile.
Hata akiba sina, siugui ovyoovyo. Siku nikitimuliwa home sijui itakuwaje[emoji22]. Japo Sir God analinda ile mbaya.
Acha kufatilia maisha ya hao marafiki zao na rika lako kwa ujumla.
Kwa kuacha kuangalia what's up status zao.(HAPA UNAWEZA KU MUTE AU UKASAVE NAMBA ZAO PEMBENI)
Kuacha kuulizia kuhusu maisha yao.
Kuacha au kupunguza kutumia mitandao ya kijamii itakayo fanya kukutana na post zao au kuona pia mfano Facebook na Instagram.
HAPO UTAKUTA MTU ANA POST YUKO KWENYE DUALIS caption Ina someka way to TANGA for weekend halafu akifika ana post nyingine akiwa kwenye restaurant Kali akipiga launch akiwa na mtoto mkali wa kidigo ana kwambia amefika salama.Muda huo wewe unapigana na shemeji akuachie ukoko wa wali siku nyingi ume umiss [emoji28]. Lazima u frustrate!!!
Focus kwenye maisha yako,maisha yako Sasa hivi ni kusoma.Hakikisha una pigana kweli kweli Kwa kupata marks nzuri kuepukana na supp zisizo za msingi ma Repeat module yasiyo na lazima hata ku disco pia na mwisho upate GPA nzuri Umalize diploma Yako fresh.
Usiache kabisa ila punguza kuwasiliana nao kama hakuna ulazima acha kabisa kuwasiliana nao,Hii itaepusha kuambiwa mipango Yao ambayo wewe itakutoa kwenye reli na kukuongezea stress zaidi.Mfano jamaa akupigie simu ana enda Dodoma kuangalia Nyumba anayo taka kununua milion 78, ana mashamba Morogoro karibia ekari 30,ana mpango wa kuongeza gari jingine mwezi wa 10 maana kluger v kaichoka na vingine vingi.
Heshimu kila mtu si mkubwa siyo mdogo na kuwa mwaminifu pia,Hii itakutengenezea kesho yako nzuri especially Kwa kupata connection Kwa future Yako mbeleni.
Wakati wa likizo ndefu unaweza kutafuta kitu Cha kukuongezea ujuzi zaidi nje ya fani unayo somea Yote ni Kwa ajiri ya kesho yako na kuacha kushinda kwenye social media kufatilia maisha ya watu Ingali ya kwako ameyashika shemeji Yako.
Epuka kumpa ujauzito mwanamke yeyote kuepusha mzigo maana wewe hapo ulipo ni mzigo Kwa kaka Yako.
Usimwamini mtu yeyote Kwa kumwambia mambo yako au mipango Yako kama hakuna ulazima wowotee wa kufanya hivyoo,Bora mnyama kuliko mtu.
kubwa kuliko ni MAOMBI,SALA NA DUA.
Lakini Kaa ukijua maisha haya formula,