Nahisi mama mzazi anadhulumiwa haki na baba?

Kig

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
1,076
Reaction score
458
baba na mama walifunga ndoa miaka karibu 40 iliyopita. Miaka 5 baada ya ndoa baba aliondoka kwenda wilaya fulani kutafuta kazi akamuacha mama yetu kijijini. Alifanikiwa kupata ajira ya kudumu kwenye shirika fulani la serikali. huko akaoa mke wa pili. tangu alipooa mke wa pili miaka ya mwanzon mwa 1980s mama yetu alimtelekeza bila matunzo yoyote hadi leo. baba Amestaafu miaka ya hivi karibuni lakini hajarudi kijijini aliko mama yetu bali amejenga nyumba kijiji cha jirani na kile anachoishi mama.

Kinachosikitisha ni kwamba baada ya kustaafu akiwa safarini huwa anapita nyumbani kwa mama yetu kumsalimia tu lakini haiingii hata sebuleni. (anaishia uwanjani tu na kuondoka). Tumepata tetesi kuwa amelipwa mafao ya kustaafu kazini hivi karibuni. hajamwambia mama yetu wala sisi watoto wa mke wake kwanza. anazitumbua tu mama mdogo na watoto wa mama mdogo. mama amekuwa akiumia sana, na bado anaumia sana kwa yale anayotendewa lakini amevumilia, ametulea mimi na wadogo zangu hadi sasa tunakazi zetu tunajitegemea na bado anaendelea kuvumilia. Binafsi naona kama vile mama ana haki ya kufaidi mafao ya mume wake wa ndoa kama anavyofaidi mama mdogo. Tafadhali naomba ushauri wenu wadau nifanye nini ili mama yangu nae apate haki ya mafao ya mume wake wa ndoa japo kidogo tu? kama mama hana haki naomba mniambie pia ili nisipoteze muda kulitafakari jambo hili. ushauri wenu ni muhimu sana.


asanteni
 
Mkuu, hingera kwa ujasiri wa kueleza ukweli. Mimi pia nafuatilia masuala ya ndoa ya baba yangu aliyeachana na mama yangu kama wewe, tofauti ni kwamba mimi baba aliamua kukaa kando baada ya ukorofi wa mama yangu na ambao nilikuja kuugundua nilipmaliza University baada ya kuniletea ukorofi uleule, nikamkatalia na hadi leo hatuelewani na mama yangu na sijali. Mimi baba alifariki baada ya miaka mitano ndoa ya mama ilipovunjika.


nikirejea kesi yako unasema ndoa ya wazazi wako ilivunjika miaka 40 iliyopita maana yake ni mwaka 1975. Kiuhalilisa ni kwamba ndoa ni ile miaka ambayo mke na mume waliishi. Hivyo, mama yako ana haki za ndoa kwa kipindi kile cha miaka mitano aliyoishi na baba yako.

Baada ya hapo yaani 1976, hakukuwa na ndoa tena. Sasa kosa alilofanya mama yako ni kwamba kama alitaka mafao basi ilibidi amshitaki baba yako ndani ya miaka kadhaa, yaani angemshitaki kufikia mwaka 1980.

Mahakama huwa zina kitu kinaitwa status of limitation yaani ukipita muda fulani unaonekana umesamehe kosa fulani, wanasema umfanya "condonation" na hivyo hutakiwi kushitaki.

Hivyo kuanzia mwaka baba alipomuoa huyo mama mdogo, serikali inatambua ndoa yake na watoto wa huyo mama mdogo, na kwa hakika ni wadogo zako.

Sasa, kama baba alipewa mafao yake, basi unachoweza kufanya ni kuangalia kwamba kile kipande cha miaka mitano alichofanya kazi huku akiwa na ndoa ya mama yako, basi unaweza kukidai kama hujachelewa.

Kama baba yako alianza kazi mwaka 1970 akastaafu mwaka jana, yaani 2014, basi mama yako apewe kipande cha mafao kwa miaka mitano, tena igawanywe kulingana na kiwango ambacho mama yako alikuwa anaigiza kipato kiuchumi. Naju awanawake wengi hupenda kusema ni nusu kwa nusu. Uongo. Nusu kwa nusu vipi wakati kuna wanawake wengine wanaingiza pato kubwa wakati wengine ni golikipa.

Lakini kwa kesi yako imeonekana kwamba baba alienda wilaya nyingine kutafuta kazi. Kumbe wakati yuko na mama yako hakuwa na kazi. Hivyo mafao ya kazi aliyopata hayamhusu mama yako bali mke mdogo na wanae.

Hayo ndiyo ninayoweza kukusaidia. Lakini baba yako kutumbua na mke mdogo na watoto wake, hiyo ni haki maana wamemvumilia huyo baba yako kwa miaka tele yaani tangu aliposhindwana na mama yako hadi leo.

Ndoa zina matatizo sana, tukiziangalia eti kwa sababu unampenda mzazi aliyekulea, unaweza kujikuta unaingia katika ujinga aliotumbukia mama yako ukaishia kupotoka kama yeye bila kujua sababu zilizopelekea kutengana.

Mimi nilijifunza kwa kupeleleza na nikamchukia mama na wajomba wengi ambao walituaminisha kwamba baba alikuwa mkosefu na ukoo wa baba wote ulikuwa ni wakorofi. Nilipotafiti nikaona kumbe ukoo wa mama ndiyo umeoza na hadi leo ninaelewana nao wale tu waliosimamia ukweli.

Tena nampongeza baba yako walau anapita sebuleni kumsalimia mtalaka wake na nyinyi watoto wake mnamuona. Mimi binafsi sina moyp huo. NIkiachana na msichana ndiyo kwa heri moja kwa moja na sihitaji nirekebishwe kwa hilo maana sintarekebika. Ndoa zinakera na kuleta machungu yasiyosahaulika milele.

Pole sana ninaelewa uchungu wa hali kama hizi. Ninawaomba wachangiaji wengine wasilete kejeli katika mambo kama haya ambayo badala ya kupoza wanazidi kuchochoea moto uhusiano.
 

nashukuru kwa kunielimisha juu ya jambo hili. Nimepata mwanga kiasi maana nilikuwa sijui kitu kabisa.
lakini Naomba nifafanue kidogo. ni kwamba baba na mama hawajaachana rasmi. Na kuna baadhi ya mambo ya kifamilia bado wanashirikiana japo kinafiki, pia jamii nzima inayotuzunguka wakiwemo ndugu wa baba na ndugu wa mama bado wanawaonda baba na mama yangu kama wanandoa maana hakuna mahali waliwahi kushitakiana kuwa wanataka kuachana au wamegombana. Nilichokiona, na ninachokijua ni kwamba baba aliamua kumtelekeza mama na sisi watoto wake baada ya kuoa mke wa pili. Je mke akitelekezwa ndio kusema ameachika au ndoa imevunjika? Na ktk mazingira haya ya kutelekezwa, mama hana haki ya kupata mafao ya mume wake?
 
Sijui kama hiyo mashirikiano ya kimila yana ridhaa ya wote baba na mama. Kama sivyo, basi ile kumtelekeza tayari hapo hakuna ndoa. Kumbuka kwamba hata kukaa vyumba tofauti na ikathibitika, basi hapo hakuna ndoa.

tena hizi za watu kulala vyumba tofauti ndizo nyigi huku mjini na hasa kama mume na mke walijenga pamoja na wana watoto.
 
Swali la msingi ni je hio ndoa ni ya kikristo au ya kiislamu, maana ndoa ya kiislamu ni potentially polygamous wakati ya kikristo ni monogamous hivyo kama ni ya kikristo mke anaetambulika ni yule wa kwanza tu
 
Swali la msingi ni je hio ndoa ni ya kikristo au ya kiislamu, maana ndoa ya kiislamu ni potentially polygamous wakati ya kikristo ni monogamous hivyo kama ni ya kikristo mke anaetambulika ni yule wa kwanza tu

ya kikristo mkuu. Je sheria nayo inamtambua mke wa kwanza pekee yake?
 
Kazi afanye baba mafao apate mama we unadhani ni haki hiyo?
 

Wote humu tungekua kama ww tungefika mbali mkuu ww una akili sana dah salute kwako bhna hv unaweza ukawa na umri gani?
 
Swali la msingi ni je hio ndoa ni ya kikristo au ya kiislamu, maana ndoa ya kiislamu ni potentially polygamous wakati ya kikristo ni monogamous hivyo kama ni ya kikristo mke anaetambulika ni yule wa kwanza tu

Mkuu anauliza kuhusu mafao kwa mujibu wa sheria za kiserikali maana hakutaja kabisa suala la dini unalolipachika wewe.

Cc:

Kig
 
We akili yako na ID yako ni vitu viwili tofauti. Ulitaka mama afanyeje ??????!! Kama una akili nzuri mama ana HAKI ya kupata chochote

Wewe mtoto wa kiume badala ya kujipinda umkwamue mama,unalilia hela ya kustaafu ya baba ako unaona ni haki?kwanini hamkushughulika naye kipindi hicho saivi amepata mafao unaanza kulia lia,wababa wengi sana wanakandamizwa haki zao siku hizi,kila mtu utasikia bila mama misingefanikia
 
We akili yako na ID yako ni vitu viwili tofauti. Ulitaka mama afanyeje ??????!! Kama una akili nzuri mama ana HAKI ya kupata chochote

Wewe mtoto wa kiume badala ya kujipinda umkwamue mama,unalilia hela ya kustaafu ya baba ako unaona ni haki?kwanini hamkushughulika naye kipindi hicho saivi amepata mafao unaanza kulia lia,wababa wengi sana wanakandamizwa haki zao siku hizi,kila mtu utasikia bila mama misingefanikia
 
Mkuu anauliza kuhusu mafao kwa mujibu wa sheria za kiserikali maana hakutaja kabisa suala la dini unalolipachika wewe.

Cc:

Kig

Wewe ilibidi uulize hio ndoa ni kwa mujibu wa dini gani maana kuna aina nyingi za ndoa ya kikristo, kiislamu, kiserikali, kimila....kwaio kuanza tu kumpa maelezo umempotosha maana hapo juu ameshaniquote ndoa yenyewe ni ya kikristo kimsingi hio ndoa ya kwanza bado ipo valid maana ndoa ya kikristo ni monogamous...1 man 1 wife...kwaio huyo mama ana haki zote juu ya hizo mali ambazo mumewe amezipata sababu ndoa ya kwanza bado inaendelea..
 
ya kikristo mkuu. Je sheria nayo inamtambua mke wa kwanza pekee yake?
Basi kama ni ya kikristo mana yake huyo mke wa kwanza hajaachwa maana ndoa za kikristo ni monogamous kwaio huyo mke wa pili anachukuliwa kama concubine ambaye kimsingi hana haki yeyote ile bali wenye haki ni hao watoto aliozaa nao kwaio bi mkubwa anaweza file for separation/divorce kwa kigezo cha desertion{kutelekezwa} na pia kunyimwa haki zake za kimsingi za kindoa...
 


Wewe ndiye unapotosha. Anepeleka suala lake kwenye mahakama ya nchi na si ya kanisa.

Cc:

Kig
 
Dingi alishatupa jongoo na kijitichake...Sasa kilichobaki mnapaswa kumsaidia mama....mmeshakuwa watoto wakubwa iweje nawewe utolee macho mafao ya mzee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…