Kig
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 1,076
- 458
baba na mama walifunga ndoa miaka karibu 40 iliyopita. Miaka 5 baada ya ndoa baba aliondoka kwenda wilaya fulani kutafuta kazi akamuacha mama yetu kijijini. Alifanikiwa kupata ajira ya kudumu kwenye shirika fulani la serikali. huko akaoa mke wa pili. tangu alipooa mke wa pili miaka ya mwanzon mwa 1980s mama yetu alimtelekeza bila matunzo yoyote hadi leo. baba Amestaafu miaka ya hivi karibuni lakini hajarudi kijijini aliko mama yetu bali amejenga nyumba kijiji cha jirani na kile anachoishi mama.
Kinachosikitisha ni kwamba baada ya kustaafu akiwa safarini huwa anapita nyumbani kwa mama yetu kumsalimia tu lakini haiingii hata sebuleni. (anaishia uwanjani tu na kuondoka). Tumepata tetesi kuwa amelipwa mafao ya kustaafu kazini hivi karibuni. hajamwambia mama yetu wala sisi watoto wa mke wake kwanza. anazitumbua tu mama mdogo na watoto wa mama mdogo. mama amekuwa akiumia sana, na bado anaumia sana kwa yale anayotendewa lakini amevumilia, ametulea mimi na wadogo zangu hadi sasa tunakazi zetu tunajitegemea na bado anaendelea kuvumilia. Binafsi naona kama vile mama ana haki ya kufaidi mafao ya mume wake wa ndoa kama anavyofaidi mama mdogo. Tafadhali naomba ushauri wenu wadau nifanye nini ili mama yangu nae apate haki ya mafao ya mume wake wa ndoa japo kidogo tu? kama mama hana haki naomba mniambie pia ili nisipoteze muda kulitafakari jambo hili. ushauri wenu ni muhimu sana.
asanteni