Nahisi mume wangu kanichoka kabisa

Kama unaweza kushare just share, hakuna anayrkufahamu humu, hatuna wataalam wa kusaidia mambo haya. The more you talk unazidi kupata relief.

I hope he'll come by na kujirudi. Wewe fanya kile unachoamini kitaleta furaha kwa familia yako.
 
Niliwahi kufungua uzi kuhusu wanawake kumove on na wasiache kazi kisa mwanaume.
 
Jaribu kumuomba usafiri uende likizo at least two months ili uwe mbali naye angalau akumiss
 
wewe unamdanganya kabisa ushauri wa hovyo huu ulioutoa japo ni haki yako kutoa naomi
 
Nahisi Tatizo ni lako,

Tafuta namna ya kuwa bize, yaani mpe nafasi ya kukumiss,

Pia Usitegemeze furaha yako kwake Find something that you love and dive into it, Just be happy and not like stressed mda wote.

Kuwa kama mwanamke anaeweza kutamanisha as before. Tatizo wanawake mkiolewa mnaacha kuvaa vizuri, hata kujiweka safi mda mwingine.
Na la Mwisho Muache Mwanaume awe mwanaume. Acha kulazimisha vitu, hata kama wazo ni lako mfanye aonekane yeye ndio kaamua na upunguze kisirani.
 
Kwenye ndoa, mmojawapo anapokosa uaminifu basi ndoa hutetereka.

Mmoja wenu kapata aliyebora kuliko mwenzake huko nje. Wandani anaonekana takataka.

Remember! Neediness is the most unattractive trait thats ruin the relationship.

Familia isiyosali/swali pamoja humkaribisha Satan miongoni mwao na ndo hapo chanzo cha matatizo huanzia.

Pole sana mkuu. Usichoke kuipambania ndoa yako.
 
Pole
 
Inawezekana hajiamini huyo mumewako!kwahiyo anakushusha ili ujione takataka zaidi.

Inawezekana pia nguvu za kiume zimeanza kupungua kwahiyo anakunyanyasa ili ukose kujiamini kabisa ujione haufai na huwezi kupata mwanaume wa kukupenda zaidi yake!yaani anakufanya uamini yeye ndio amekustiri wewe[emoji23]bila yeye huwezi kuishi[emoji23]!

Unyanyasaji ni miongoni mwa mbinu wanayoitumia wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume ili usiweze KUMUACHA!!,wanakua na shida sana!ubabe mwingiii,amri nyingi ndani tena za ajabu ajabu,mkali sanaa,matusi mengiii,mwingine hata kukupiga anaweza kukupiga

Kama nguvu zake ziko sawa basi huyo mtu ana mwanamke mwingine!!mimi nilipitia situation kama yako!tena hivyohivyo kabisa!ni amini mimi jamaa ana MTU WAKE!wanaume wengine hawawezi kubalance upendo hivyo anaegemea sana kwa mchepuko kuliko kwako!

Kama amekuchoka kweli basi hakuna namna yeyote ile unaweza kufanya ili akupende tena!yaani wanaume wakikuchoka wanakua hivyo!Kuna njia 2 za kufanya nazi ni hizi;

1.Kama munayo ndoa ya kanisani basi na munaowatoto kama ulivyosema basi wewe anza kuhangaika na watoto wako!una degree moja (kama nimekuelewa vizuri)toka ndani nenda katafute ajira hata kwenye viwanda,makampuni na mashirika binafsi,usichoke utapata tu nakuombea!

2.Acha kabisa kumfata fata!Mahaba ni Intimacy lakini Intimacy hiyohiyo inageuka kero pindi mapenzi yanapokufa,Nakuelewa!Najua ni ngumu sana kuacha kumfatilia au kujipendekeza kwa mumeo hasa kama unampenda sana!ila jitahidi hivyohivyo kidogokidogo utaweza

3.Usitegemee yeye kubadilika,wewe ndie ubadilike!
Amua kuchagua furaha,hata kama kwasasa huna hela ya kujiremba ila nina Imani unazo nguo nzuri kabatini,Oga vizuri na Ubane/Chana nywele zako vizuri..Hakuna Tiba kubwa zaidi ya Tabasamu!!Mylove Tabasamu!!ni ngumu kutabasamu ikiwa moyo unavuja damu ila jitahidi tu!![emoji30]Usionyeshe unyonge ukiwa nae,Acha kulalamika.

4.Jenga imani kwamba huyo sio wako tena!kubali kuachika!Ona kama jamaa anakusaidia tu wewe na watoto wako kwa muda mfupi kabla hujaachwa Officialy!!ukijijengea dhana hii itakua msaada mkubwa kwako wa kumove On haraka na kupooza moyo wako!

5.Mwisho!usimuache mungu,Omba mungu akupe moyo wa kuishi bila yeye na sio mungu ambadilishe yeye!

Natamani ningekuwa karibu na wewe tukashare maumivu na uzoefu maana njia yetu moja!
 
Tatizo lipo kwenye chanzo cha kuaona kwenu.

Imeandikwa;

“Enyi binti Sayuni msiyachochee mapenzi mpaka yatakapoona yenyewe kufaa”

Mwanamke kumshinikiza Mwanaume akajitambulishe kwenu kisha atoe mahali akuoe bila yeye mwenyewe kuamua kufanya hiyo juhudi matokeo yake huwa kama hayo [emoji108]

Na wengine huenda mbali kwa kuwaroga wachumba zao kwa kuwapumbaza akili wawaoe haraka.

Baada ya muda matokeo huwa hayo.

Tafakali.

Actually sio wewe tu wanawake wengi wanakutana na hali hiyo kwa nyakati tofauti tofauti.

Wengine wanaishi kinyume na nature , wanawatala wanaume wao ndio wana kauli ya mwisho kwenye Nyumba baada ya muda matokeo huwa kama hayo Mwanaume akichoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…