Wanajamvi,
Naishi katika nyumba ya kupanga na tumepanga familia tano mwenye nyumba anaishi mbali,alianza mpangaji mmoja kuugua miguu.
Yaani inauma kama inachomwa moto, baada ya wiki mbili wife nae miguu ikaanza, baada ya wiki mbili na siku mtoto wangu nae ikaanza pia na mimi naanza kuisikia imeanza kuuma kwa mbali.
Pia yule mpangaji aliyeanza kuugua ni best wa wife wangu, na kwa sasa hata kutembea ni shida, pia mtoto wangu ndo kaanza kuongea usiku hatulali ni kulia tu, na anasema 'miguu oto' akimaanisha miguu inawaka moto, nifanyeje?
Sina kifurushi nitarudi kesho asubuhi