Nahisi nalogwa na mchawi

Nahisi nalogwa na mchawi

napenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
485
Reaction score
90
Wanajamvi,

Naishi katika nyumba ya kupanga na tumepanga familia tano mwenye nyumba anaishi mbali,alianza mpangaji mmoja kuugua miguu.

Yaani inauma kama inachomwa moto, baada ya wiki mbili wife nae miguu ikaanza, baada ya wiki mbili na siku mtoto wangu nae ikaanza pia na mimi naanza kuisikia imeanza kuuma kwa mbali.

Pia yule mpangaji aliyeanza kuugua ni best wa wife wangu, na kwa sasa hata kutembea ni shida, pia mtoto wangu ndo kaanza kuongea usiku hatulali ni kulia tu, na anasema 'miguu oto' akimaanisha miguu inawaka moto, nifanyeje?

Sina kifurushi nitarudi kesho asubuhi
 
Wenzenu (wachawi) wanafanya hiyo miguu yenu kama kuni. Mpeni Yesu maisha. Ipo siku mtalalamika vichwa vinawauma sana.
 
Hahahahahaha nim2heka sana heti "mtoto wangu ndo kaanza kuongea usiku hatulali ni kulia tu, na anasema 'miguu oto'"
 
Mnamshauri ahame nyumba wakati hapa kwenyewe amesema hana kifurushi!!
 
Mganga wa kienyeji sio jibu la matatizo yako,ni YESU pekee ndiye suluhisho la matatizo yako.mwamini na umuombe yeye kwa moyo wote atakuponya.
 
Mganga wa kienyeji sio jibu la matatizo yako,ni YESU pekee ndiye suluhisho la matatizo yako.mwamini na umuombe yeye kwa moyo wote atakuponya.

Mimi ninaamini uwepo wa mizimu, au uwepo wa roho za waliotangulia, dini zililetwa na waliotaka kututawala na kutuiaia, dawa ya moto ni moto na dawa ya maji ni maji, ngoja nijaribu tuone
 
Back
Top Bottom