Nahisi nimekua addicted na huu mchezo wakuu

Nahisi nimekua addicted na huu mchezo wakuu

Itakuwa wewe ni FBI ama CIA agent basi tu hujabaini hilo. Jasusi mbobezi
 
Vipi biashara zako unazifuatilia vizuri lakini?
 
Watu wafupi mara nyingi wanahii tabia (psychological problem). Am just saying, ni utafiti.
 
Ama kweli hii ni home of great thinkers...

Jomba tangazo lako limekaa kitaalamu sana.

Fanya malipo ya tangazo kwa moderator yeyote aliecactive muda huu.
 
Habari za majukumu wakuu, mimi ni kijana wa miaka 29. Nina shida moja ambayo nahisi imekuwa kama "addiction."

Nimejipata nikiwa na tabia ya kufuatilia (track) simu za kila mpenzi ninayeingia naye kwenye mahusiano, iwe nina mipango ya baadaye naye au hata kama ni uhusiano wa muda mfupi. Ilimradi tu tunakuwa na uhusiano wa kimapenzi, lazima nifuatilie mawasiliano yake. Pia, sijawahi kuwa na mahusiano mafupi; karibu mahusiano yangu yote nimekuwa nikifanya hivi.

Hua nahisi kama nafurahia kufuatilia mawasiliano ya mpenzi wangu, ingawa tangu nianze kufanya hivi ni mara moja tu, mwaka 2020, nilipokutana na ujumbe uliothibitisha kuwa mpenzi wangu alikuwa amenisaliti. Wapenzi wengine wote, pamoja na huyu niliye naye sasa, sijawahi kuona dalili yoyote ya usaliti.

Natamani niache hii tabia, lakini nahisi nashindwa. Najikuta natoa "tracker," lakini baada ya muda mfupi nairudisha tena. Nahitaji ushauri wenu juu ya hili. Nitashukuru sana.
Hongera kwa tangazo
 
Back
Top Bottom