Nahisi nimepigwa kwenye hizi spare nilizoandikiwa

Soma umuelewe jamaa alipeleka kwa nia njema kabisa! Sasa yamemkuta mpe moyo mwaka mpya huu tuanze salama, au we mgogo?πŸ€”πŸ€”πŸ€”
Mimi concern yangu ni kwamba kwa nini mtu uende kwa Daktari kisha umpangie daktari magonjwa ya kutibu badala ya kumwambia Daktari akucheki kisha akuambie tatizo?

Naandika haya ili kusaidia watu wengine pia kuwa wanapoenda garage wasiwapangie mafundi kubadili spea bali waache mafundi wafanye kazi yao inayowaingizia kula kila siku ya kucheki matatizo ya gari kisha mafundi watasema wenyewe tatizo ni nini.
 
Mkuu hawa mafundi wetu usipowapangia na usipokuwa makini, watabadilisha mpaka siti yako wakuwekee kigoda...
.tatizo mafundi hawana weledi wa kutosha. ...na wale wenye weledi, wengi wao wanaringa na kuwaachia manyoka kazi ili wao waonekane ndiyo maboss..

Kwa mimi, fundi hawezi kuniambia ninunue spea fulani bila yeye kuitoa tuikagie wote, ikiwezekana tunashirikisha na mafundi wwngine
 
Ushauri mzuri sana kabisa huu, yaani break shoo na break pads tena zinahusikajae hapo kwenye gari kupiga kelele.
 
Break pad za IST Elf 65?? Kudadeki

Shock up 2 za nyuma 140?
 
Shock up mbele 1pcπŸ˜€πŸ˜€ huyo fundi wa wapi anaebadilisha shock up ya upande mmoja? kituko..... hizo huwa zinabadilishwa kwa pair ili ziwe na same tension...
 
Ulivutiwa na jina nini ukajua ni Japan penyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…