Nahisi nimetongoza jini

Nahisi nimetongoza jini

dawa yenu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
2,825
Reaction score
3,675
Hakika kilikuwa kipindi kigumu sana ila alhamdulillah kimepita salama na sasa maisha yanaendelea.

Tuachane na hayo, tulijadili hili ninaloliwasilisha hapa jamvini.
Mwenzenu huu msimu wa uchaguzi umekuja na neema zake.

Licha ya kwamba jembe langu halijaingia mjengoni ila angalau nimepata cha kuipooza nafsi yangu na kunisahaulisha dhahma zote nilizokumbana nazo wakati huu mfupi.

Nimepata kigoli kimoja matata sana. Kimeumbika hakuna mfanowe, kina rangi ya mtume, hiyo sauti sasa mmh... mtoto jicho jicho, akinichumu utamu naona mimi.

Mtoto ametimia ndani na nje, mpole, mkarimu na zaidi ya yote mcheshi kwa kila mtu. Ila yote tisa kumi ni hili.

Huyu mrembo nashindwa kumuelewa kabisa. Ananitisha yaan naanza kumuogopa kwa kweli. Mambo yake yanastaajabisha. Ni mpenzi wa movie. Hilo si tatizo ila tatizo ni aina ya movie anazopenda.

Anapenda movie za kutisha tu. Mara watu wanachinjana, mara huyu kamnyofoa mwenzake koromeo, mara yule anatafuna gegedo la mwenzake, mara huyu kampasua mwenzake kichwa halafu anakunywa ubongo!! yaani taabu tupu.

Hivi hapa saa hizi anaangalia final destination amezipanga ya kwanza hadi ya tano, haogopi. Na kaniambia haimsisimui sana. Aisee!

Muonekano wake na aina ya movie anazotaka ni mbingu na ardhi abadani havifanani.

Huyu ilibidi awe anaangalia movie za kifilipino za akina Angelo, au zile za kizungu zile nyepesi nyepesi .

Muenendo wake unanitisha, nisije nikawa nimetongoza jini. Asije akaninyofoa uhai huyu.

Naombeni ushauri wanajamvi maana nimechanganyikiwa.
 
hahaaaa unaogopa ukimuudhi utakuta kakata gegedo
 
Mi mwenyewe napenda za mazombie na mavampire za kifilipino hapana
 
huyo ndio mwenyewe sasa sio hawa wa drama
 
sawa tumekuelewa kua una mwanamke mzuri
 
Back
Top Bottom