#COVID19 Nahisi nina Covid 19

Usiache kufukiza walau mara mbili kwa wiki.

Ushauri wa Wakulungwa hapo juu pia inahusika.
1.pima
2. pata vit c kwa wingi
3. pata zinc
4. pata antibiotics
5. pata predinisolone
ANGALIZO: Hizi dawa upate toka kwa Mtaalam wa masuala ya Afya (Daktari).

Pia usiache kufanya mazoezi.

Epuka pombe, sugars kwa wakati huu mpaka upate nafuu.
 
Ukiumwa wewe inatosha hiyo Corona inatosha.
Korona ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine msituletee mayowe yasio na maana

Korona ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine 🤣 ugonjwa gani huo? Jifanye mjanja, tena inapenda watu wabishi wabishi kama ninyi
 
kama uko kwenye mikusanyiko au msongamano wa watu halafu hujavaa barakoa halafu ukaambukizwa kirusi cha korona halafu ukafa, hapo nani wakulaumiwa?
je kunahaja ya kumlilia mtu aliye hatarisha uhai wake kwa uzembe wake mwenyewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Mkuu chukua ushauri wa wadau hapo juu naona wameelezea vizuri sana...
 
Pole sana,Pamoja na ushauri toka kwa wadau hapo juu... Muombe Mungu akuvushe salama katika kipindi hiki kigumu,Ugua pole ndugu!!
 
Your browser is not able to display this video.
Kupima corona ni gharama. Hapa kwenye video tunaweza pata kitu cha kujifunza katika kupambana na Corona, lakini pata ushauri wa daktari.
 
Mkuu tafuta tangawizi, malimao na asali chemsha vichanganyike vzuri(wauza tangawizi pia wanayo) tungeneza ile kali kunywa siku mbli mfululizo au zaid utakuja kunishukuru badae
 
Kama rais anakusanya watu ili awaambie wasikusanyike unategemea nini?

Makala jana kakusanya umati mbezi. Hawa wanasiasa ndio wapuuzi sana. Badala wawe mstari wa mbele kutoa elimu kwa raia wao ndio kwanza wanawakusanya.

Hatari sana
 
Andika vizuri hizo dawa jombaaa watu tuzame pharmacy
 
Duu mmepaniki wakuu mbona comments mnaandika kwa kuchapia sana.
 
MKUU..KUJIFYKIZA SI WATU WALISEMA NI USHAMBA WA MAGUFURI NA WOTE HUMU TUKAKUBALIANA NI UWONGO NA USHAMBA AU TULISEMA KUMCHUKIA BURE HUKU TUKIAPPRECIATE MAMBO YAKE

Pamoja na ushauri woote wa wadau hapo juu pia usisahau kujifukiza
 
Unatakaje boss? Kisa unaumwa tufunge mtaa
Watu tumekuwa waoga sana, utadhani hatutakufa, kwani korona ndio imeanza mwaka huu? kama mtu anaogopa korona ahamie porini akaishi na nyumbu.
 
Fatilia michango yangu mie ni team mwendazake lia lia huwezi niambia kuhusu chanjo ila kujifukiza na kjnywa tangawizi na malimao nipo hapo
MKUU..KUJIFYKIZA SI WATU WALISEMA NI USHAMBA WA MAGUFURI NA WOTE HUMU TUKAKUBALIANA NI UWONGO NA USHAMBA AU TULISEMA KUMCHUKIA BURE HUKU TUKIAPPRECIATE MAMBO YAKE
 
Hospital kufanya nini, kunywa dawa, tafuta erythromycin mg 500, vidonge vya vitamin C na Asprin
 
Umetumia nyungu? au umefuata akili za makuwadi wa mabeberu kwamba nyungu haifai....
 
Imooooo!! Fanya mazoezi ya kutembea na utoke jasho sana,tafuna tangawizi ,kula machungwa , mananasi kwa wingi Kitu cha DELTA hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…