50thebe
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 4,088
- 4,059
Usiache kufukiza walau mara mbili kwa wiki.Kwa hali niliyonayo nahisi hii ni covid 19 3rd wave Delta.
Kwa muda wa wiki nzima hii inayoisha kesho nimekua naumwa ugonjwa usiojulikana. Nimeenda hospitali zaidi ya 2 bado sionyeshi ugonjwa wowote.
Kuanzia jumamosi iliyopita nilikua naumwa kichwa kisicho cha kawaida, nikapewa dawa za kutuliza maumivu lakini wapi, jumatano nikaenda hospitali nyingine nikabadilishiwa dawa kichwa kimeacha kuuma ila mwili hauna nguvu, nimekua mnyonge na dhaifu sana.
Sina ladha ya chakula na wala sitaki kula, nataka muda wote niwe nimelala hadi mbavu zinauma, sihisi harufu yoyote lakini pia nimeanza kuhara mara moja moja na kukohoa kifua kinawasha washa.
Naomba kufahamu hapa Dar ni wapi naweza kwenda kupima covid. Ingawa nimeanza kuona improvement lakini natamani nipime niwe na uhakika.
Ahsante.
Ushauri wa Wakulungwa hapo juu pia inahusika.
1.pima
2. pata vit c kwa wingi
3. pata zinc
4. pata antibiotics
5. pata predinisolone
ANGALIZO: Hizi dawa upate toka kwa Mtaalam wa masuala ya Afya (Daktari).
Pia usiache kufanya mazoezi.
Epuka pombe, sugars kwa wakati huu mpaka upate nafuu.