Nahisi sina bahati na biashara

Nenda kwenu ukaage wazazi na ndugu wao huko nyuma ndio watakutengeneza tatizo hamuagi mnapoenda miji ya watu, hakuna aliekuuliza umeaga kwenu?
Mkuu nilikua dar nina biashara flani ikafa nikaamua kuingia mkoani kusaka life nikaanzia tunduma mambo sikuyaelewa nikaenda mgodini chunya huko mambo sikuyaelewa pia nikaamua kuja mwanza nikaanza hii biashara nayenyewe ndio hivi yani acha tuu, toka dar watu wananiambia niende home nipate baraka ndio nirudi kupambana itabidi niende mkuu coz mara ya mwisho home nimeenda 2015.
 
Nenda kwenu ukaage
 
Nenda lindi au mtwara chukua ekari 5 anza ufugaji wa mbuzi na kuku wa kienyeji. Hakikisha unalima miti ya kukusaidia kulisha mbuzi wakati wa kiangazi. Weka makazi yako hapo usitake kufanya kilimo cha m Pesa na simu, kaa hapo mwenyewe hata mwaka mzima.

Kama unatumia kitimoto nenda sehemu yoyote wanapolima mahindi kwa wingi fuga kitimoto jike 8 dume wawili baada ya mwaka mmoja utanishukuru

Wakati unaendelea na ufugaji lima pia mahindi na maharage

Samaki mimi huwa sizielewi kabisa
 
Mkuu tafuta mfanyabiashara mzoefu wa hiyo biashara yeye ndo akufundishe njia za kupita. Ni mara chache sana utatoka huko tu na pesa zako uingie kwenye biashara na kujua siri zake bila kupoteza fedha au kumaliza mtaji wote kabla hujakaa sawa.
 
Uwe unatenga pia muda wa kutosha wa kukaa peke yako na kutafakari, siyo muda wote upo Facebook, siyo muda wote upo na simu, huwezi kufanikiwa hivi. Tenga muda dakika 60 kila siku ukiwa peke yako bila simu wala distraction yoyote utaona majibu ya maswali yako yanakuja Yenyewe
 
Mkuu watanzania tuna roho mbaya sana yani mtu anaconnection ya wavuvi visiwa tofauti unamuomba akuunganishe nao uwalete anakukazia, mkikutana utasikia vipi mzee bado hujaanza kukusanya mzigo? Yani full unafiki na roho mbaya.
 
Nimekua interested na comment yako but mataji nishaupunguza ngoja nijichange tena, heka moja huko bei gani?
Inategemea, kuna mashamba pori ambayo unasafisha wewe kwa mara ya kwanza unaweza kuuziwa elfu 50 au elfu 30 kwa ekari au ukimuona mwenyekiti wa kijiji ukimpa kitu kidogo anaweza Kukuambia ujikatie unapoona utapaweza, na ndani ya mashamba haya kuna kuni bila idadi pia mkaa bila idadi

Lindi, mtwara, pwani bado ardhi ni bei sawa na BURE

NB: Nimekupa wazo ila mimi sina connection yoyote lazima ujiongeze mwenyewe
 
Shukrani mkuu, barikiwa.
 
Mkuu watanzania tuna roho mbaya sana yani mtu anaconnection ya wavuvi visiwa tofauti unamuomba akuunganishe nao uwalete anakukazia, mkikutana utasikia vipi mzee bado hujaanza kukusanya mzigo? Yani full unafiki na roho mbaya.
Hili ni tatizo jingine na tatizo kuu ila sasa hakuna option ts either uwe na mtu wa kukuonyesha njia au utumie pesa nyingi kufanya uchunguzi na kutengeneza network.
 
Uwe unatenga pia muda wa kutosha wa kukaa peke yako na kutafakari, siyo muda wote upo Facebook, siyo muda wote upo na simu, huwezi kufanikiwa hivi. Tenga muda dakika 60 kila siku ukiwa peke yako bila simu wala distraction yoyote utaona majibu ya maswali yako yanakuja Yenyewe
 
Gem tafu....jamaa wanamkataa lkn yy hajui kama wamemkataa inabidi atulie ausome mchezo kwanzq apeleleze atapata majibu. Biashara yyte kama huijui usikurupuke jifanye fala.....angeingia hata kwenye kuomba kibarua cha kutumwa kuvua ili azisome ABCD
Huu mkakati ulikuwa mzuri yaani angetuliza mtaji wake sehemu kisha angeingia front kama chambo baadae ndio angeibuka, sasa hivi kaonekana mvamizi. Nimejifunza kitu hapa
 
Hili ni tatizo jingine na tatizo kuu ila sasa hakuna option ts either uwe na mtu wa kukuonyesha njia au utumie pesa nyingi kufanya uchunguzi na kutengeneza network.
Mkuu kuna watu washatengeneza connection yani wao hata visiwani hawaji wapo mwanza kwa siku wanatumiwa mzigo wa zaidi ya 1m kutoka visiwa tofauti tofauti sema wamewemeza pia kwenye uvuvi.
 
Mkuu kuna watu washatengeneza connection yani wao hata visiwani hawaji wapo mwanza kwa siku wanatumiwa mzigo wa zaidi ya 1m kutoka visiwa tofauti tofauti sema wamewemeza pia kwenye uvuvi.
Hapo inabidi utumie fedha kutengeneza network taratibu mpaka na wewe uzoeleke sababu mara nyingi wanaogopa kumkimbia kwa haraka aliyefanya nae muda mrefu na kumfata mtu ambaye hana uhakika kama atakuwepo kwa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…