Nahisi sina bahati na biashara

Uganga ni maarifa yaliyoumbwa na mungu waliyonayo wanadamu .kinachoponya TV ni ufundi wa kutengeneza TV sasa ww TV imeharibika Anza kusema maarifa yote ya mungu uanze kuomba mungu .acha ujinga nenda kwa fundi TV dakika tano TV inapona.
Ndio nimekwambia hata huyo fundi TV anamuomba Mungu TV ipone Mungu akitia lock hata fundi aweje TV haiponi
 
Biashara yoyote unayoanza na kuanza kukupa faida papo kwa papo, haiwezi kukutajirisha, utaishia kupata vichenji vya kula tu, huwezi piga hatua zaidi..! Biashara za kukupa utajiri huwa ni ngumu sana unaweza fanya mwaka mzima huoni faida zaidi ya kutumia tu, ila siku ikianza kukulipa utajiri huo hapo. Watu wengi huwa wanachemka kwa kukosa focus and Consistency, wewe mara umeenda chunya ukakimbia, mara tunduma ukakimbia tena....! Utajikuta miaka inaenda hakuna cha maana umefanya, utatafuta mchawi wako ingali mchawi ni we mwenyewe....! Kuna siri kubwa kwenye kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu mpaka upate matokeo chanya acha kuruka ruka, tafuta kitu kimoja pambana nacho mpaka kieleweke....! Sasa mwezi mmoja tu unataka biashara ianze kukulipa kweli, bado una vingi vya kujifunza kwenye hiyo biashara tofauti na kuwaza faida kwanza
 
Mkuu nimekuelewa mpaka nimepitiliza, barikiwa sana.
 
Siku ya kwanza kujifunza self defence nikaelewa why Kuna master wa kungfu
 
Acha kujitetea mtaji umeshaubugia wewe.

pesa ya mtaji tamu sana ile chomoachomoa kidogo kidogo..ukija kushtuka dah kwisha..
 
Uza hata chai hapo fungua mgahawa wa kishkaji kupika vuta Dada mmmoja
Nenda na mda usisubiri mvuvi aje akupe dili la samaki
Na hao samaki na chapati na mimi ntakuja
 
Hebu nikwambie jambo ambalo huenda hakuna mtu atakayekuambia...

Uvuvi na madini ni kazi zinazohitaji uwe na uimara wa kiroho...

Ikiwa umetoa Hela na ahadi ya bei nzuri na bado huoni watu kukuchangamkia, ni ishara nyota Yako haiko sawa...

Kazi kama hizo unakuta kuna wafanyabiashara umewakuta, sio rahisi wakuache ufanikiwe kirahisi.

Ungejitahidi kuogea chumvi ingekusaidia.

Biashara yoyote bila Imani dhabiti kamwe hufanikiwi...
 
Nakubaliana na wewe mkuu, vp chumvi ya mawe pekee itasaidia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…