Huwa natumia sana mtandao wa Tigo. Leo asubuhi kama sa nne hivi nikanunua kifurushi cha intanet GB 1 ( huwa napata pia dk 30 kupiga mitandao yote).
Cha kushangaza/kusikitisha mda mfupi uliopita naangalia salio la kifurushi hiki, nakuta MB 800 zimeyoyoma. Sijaangalia hata video moja.
Kipindi cha nyuma, kifurushi kama hicho nlikuwa nakaa nacho hadi siku nne. Kwa kasi ya namna hiki kifurushi kinavyotembea, sa kumi ntakuwa naingia tena sokoni kununua kifurushi kingine. Hii inauma sana.
Itoshe tu kusema kuwa, vita vya Urusi vimeleta balaa kubwa. Kumekuwa na uhaba hadi wa intanet kiasi kwamba hii kidogo iliyopo inaenda kwa kasi kubwa sana.
Tuendelee kuhesabiwa kwa ustawi wa wananchi (wenye nchi?)