Week kadhaa zilizopita katika mishemishe zangu nikapata kama 6M iv, kuna vijana wenzangu ni bodaboda na kituo chao ni karibu na sehem ninayofanyia shughul zangu. Ni mara kadha wamekuwa wakinifuata kuomba niwanunue pikipik za mkataba wapo kama watatu ivi wenye huo uitaji na kila mtu alikuwa anakuja kwa mda wake.
Sasa basi baada ya kupata hicho kias nilikuwa na option kadhaa za kuiwekeza hiyo pesa ili angalau izae. Ya kwanza ni ilikiwa niitume nyumban Chunya huko kuna biashara ambayo kwa mtaji wa 6M basi ingeniletea si pungufu ya 12M baada ya miez Minne mpaka mitano, Option ya pili ilikuwa hiyo ya kujaribu kukwamuana na hao vijana wenzangu kwa kuwanunulia pikipik za Mkataba. Nikaamua kujaribu kitu kwa kununua pikipik moja tuu Kwa gharama ya 2.7M kwa mkoa wangu zinaenda kwa Bei hiyo King Lion 9a, na nikamkabidhi kijana mmoja wapo kwa makubaliano ya 10k kwa siku na Mkataba ungedum Miezi 14. Kias kilichobaki nikakituma Huko Nyumbani moja kwa moja kwa ajili ya hiyo biashara.
MREJESHO
Week tatu za mwanzo kijana wa Bodaboda alikuwa na marejesho mazuri yasiyo na Tabu hata kidogo, Baada ya hapo akaugua na zikapita Week 3 hajaingiza hata Mia kwenye Account, na mara zote nikiwa nawasiliana nae kujua hali yake aliendelea kusema ni mgonjwa na kazi angeanza Kesho, mara kesho, Mara kesho. Kesho zikawa nyingi mpaka nikachukia na yeye akajua bro kachukia na akafanya maauzi haya. Ikabid nichukue pikipik ila mpaka hapo tayar kashanitia sumu kwenye hii biashara, Naona kama nimepoteza pesa bure tuu.
Wakati kile kias kilichobak 3.3M nilikiweka kwenye ile biashara na Kimezaa 7.5M na iko Bank saiv. Labda atokee wa kunibadili mawazo ila sitak tena hiyo biashara, na hata wale wawili imebid nimpe mmoja wapo huki natafuta mteja