Mkuu shukrani sana kwani swali lako limekuwa ndiyo jibu la swali langu.Kumbe starter motor ndiyo huwa inaenda kuizungusha crank shift mpaka pale ambapo engine inaenda kwenye stage ya tatu ya combustion ambapo huwa inaweza kujitengenezea nguvu yake yenyewe ya kujiendesha.
Lakini sasa bado kuna swali limebaki kichwani.Tunajua kuwa kwenye stage ya tatu ya engine,combustion huwa inatoa nguvu inayosababisha piston kushuka chini kwa ajili ya kuendeleza mzunguko wa crank shift.Sasa nguvu ya kuirudisha piston juu kwa ajili ya exhaust stage pamoja na kurudia mzunguko mzima wa kuanzia stage one ya intake huwa inaendelea kutoka wapi?