Nahitaji Chumba cha kupanga Vikindu Dar es Salaam

Anigrain

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
1,680
Reaction score
4,204
Wakuu poleni n majukumu na kheri ya Christmas na mwaka mpya

Aisee nahitaji Chumba cha kupanga maeneo ya vikindu Mkoani Dar, ambacho either ni Masters/chumba na sebule/chumba sebule na jiko, napendelea zaidi nyumba mpya au ambayo bado inavutia, sifa za chumba kiwe na gypsum,tiles, madirisha mazuri, ndani ya Fence na pia Feni ni sifa ya ziada tu.

chumba kiwe maeneo ya vikindu center pale pale isiwe mbali sana ili kuwa karibu na sehemu ya kutafutia ridhki lakini pia kupunguza gharama na usumbufu kwenye issue za usafiri.

Nimejaribu kutafuta kwa week Sasa ila imekuwa ni ngumu kupata kutokana na mie kutokuwa karibu na eneo husika, lakini pia madalali wa vikindu bado wanafanya kazi kizamani tofauti na sehemu zingine, kwingine madalali hufungua account katika mitandao ya kijamii na kupost nyumba/vyumba vyao hivo inasaidia kuokoa muda na kupunguza usumbufu.

Kwa Baba mwenye nyumba/dalali ambae una chumba chenye sifa hizo basi nicheki DM tufanye mawasiliano, au ata kama we huna nyumba na pia sio dalali ila unamfahamu mtu ambae ana nyumba na anapangisha maeneo hayo basi ningeomba pia msaada wako.

Natanguliza Shukrani
 
Kwa taarifa tuu vikindu sio dar. Ipo wilaya ya mkuranga mkoa wa pwani. Mm siishi mkoa wa pwani ningekusaidia
 
Watu mnapapenda dar,vikindu sio dar
 
Nisaidie kushare umepata chenye sifa zipi na kodi kiasi gani.

Natanguliza shukrani
Mkuu samahani nimechelewa kuona quote yako hivo najua naweza nikawa nimekuferisha kwa namna moja au ingine

Anyway, nilipata nyumba mpya ambayo ndio imeisha kujengwa Kwa ajili ya kupangisha

Ikiwa na sifa zifuatazo
1.Chumba na sebule, chumba master's
2.Tiles
3.Choo cha Nje
4.Gypsum
5.Alumium window
6.umeme unajitegemea
7.Maji unajitegemea
8.Fence


Kodi kwa mwezi ilikuwa ni 120000
 
shukrani mkuu nimepata chumba na sebule master, kwa laki 1 maeneo ya mzinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…