Nahitaji 'Critical Thinking' katika Kulijadili Tukio Baya la Jana Kawe Maringo

Nahitaji 'Critical Thinking' katika Kulijadili Tukio Baya la Jana Kawe Maringo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kutokana na Unyeti wa hilo Eneo na maeneo mengi ya Kawe ambayo kwa 75% yanazungukwa na hata kukaliwa na Majeshi yetu JKT na JWTZ naomba GENTAMYCINE niwe muwazi kuwa siamini na nakataa kuwa Wahusika ni hawa Panya Road tunaowaimba kila Uchao.

Inakuwaje Eneo lililotokea Tukio Baya jana liwe na Nyumba (Kaya) nyingi vile ila ilengwe tu ile (hiyo) Nyumba?

Ukichunguza Kiumakini utagundua kuwa kuna Uwezekano mkubwa Tukio Baya la Jana ni la Kifamilia (Kiundugu) ambalo limetawaliwa na Kisasi na Kukomoana.

Haya 'Critical Thinking' yangu GENTAMYCINE imeanza hivi nawaomba nanyi pia mje na zenu ili mpaka mwisho tuweze kupata Picha na hata Kiini cha tatizo na Suluhu yake pia.

Poleni Wafiwa kwa huo Msiba.
 
mimi ningekuwa IGP ningeua panyaroad kama 10 hivi! halafu ningeita ndugu! wananionyesha kwao nabeba maiti naenda tupa mtaani kwao! baada ya hapo ningesubiria mrejesho
Dunia haitaki hivyo unapaswa uzingatie haki za binadamu maana hadi kuibuka kwa hao panya road ni matokea ya mifumo..
 
Mimi nilikuwa nimekaa sebuleni nanyonya askrimu ya ukwaju mke wangu anazitengeneza anauza nilikuwa naangalia tamthilia nilivyoskia tu panya road wapo jirani nikajificha nyuma ya mke wangu na watoto wangu nilianza kulia maana nilijua huu ni mwisho wangu

Wanaume wa dar tunapitia magumu sana serikali itulinde jamani
 
Haya mambo ya panya road yamekaa kisiasa zaidi....kuna watu wanakomaa kumchafulia mama, na sisi tumewapa ahadi....
Basi wewe ndio unapotezwa na hizo habari, hapa hamna kumchafua mama wala nini. Ni tukio linatengenezwa kweli na kwa vitendo ili liwahamishe mawazo wananchi kwa hali ngumu iliopo sasa.

Ruzuku ya mafuta imeondolewa na bei imerudi kupanda, sasa matukio kama haya yanafanywa makusudically kuwapotezea focus kwenye vitu muhimu vya maisha ambavyo serikali inavifanya ....tafakari kuna mengi humo kwenye panya road hawa fake.
 
Kutokana na Unyeti wa hilo Eneo na maeneo mengi ya Kawe ambayo kwa 75% yanazungukwa na hata kukaliwa na Majeshi yetu JKT na JWTZ naomba GENTAMYCINE ...
Issue pia ni hawa wa JKT na JWTZ hawaishi katika maeneo haya pia? Kituo cha polisi cha kawe? Lugalo golf course, Lugalo penyewe?
 
Back
Top Bottom