Thanks mkuu... Nisaidie bei zile zinazofanyiwa marekebisho hapa Tanzania
Sijajua kuwa kuwa unaitka iliyofanyiwa marekebisho ya namna gani!
1.
Kuna zile mtu anaagiza kichwa cha lori (tractor unit) kutoka ulaya chenye axle conf ya 6×2 ikiwa na mid lift unaileta bongo kisha unaipeleka kwa fundi wanatoa ile axle ya nyuma wanaziacha zile mbili stable axle na ile iliyokua midlift baada ya hapo wanarefusha chasses na kukufungia nyuma axle mbili za jumla ya tairi 8 ambapo axle moja itakua ndio ina Diff.
2.
Kuna ile unaagiza ulaya kichwa kile chenye 4*2 kisha unakuja kukifanyia mchakato kama wa namba 1 hapo juu hivyo utaongeza jumla ya axles 2 ambapo moja itakua mbele na mbili zitakua nyuma na ukumbuke hizo axle za nyuma zinakua ni single diff yaani 8×2 japo ukitaka mbwembwe au kutokana na nature ya matumizi yako unawsza kutia double diff.
3.
Kununua ulaya kipisi (rigid) cha 4×2 au kile cha 6×2 ama cha 6×4. Ukichukua hicho kipisi cha 4×2 basi utaongezea eaxle moja inayokata kona pale mbele na huku nyuma utaongezea axle ya kawaida moja na kuifanya iwe mende. Kama 6×2 au 6×4 basi utaongezea axle moja tu ya kukata kona pale mbele. Na kwa hivyo vipisi unaweza kuviongezea urefu kama vitakua ni vifupi ili kukidhi mahitaji ya body ya mozigo.
4.
Kununua mende tipa kisha kuja kuvua ile body ya tipa kisha kuijengea body ya mizigo ya kawaida.
GHARAMA.
Hapa gharama zinatofautiana baina ya fundi na fundi ama eneo moja na jingine. Maeneo maarufu yenye wataalamu wa kufanya modifications hizo hapo juu ni Dar, Moshi na Arusha japo Mwanza na Dodoma nao naskia kwa sasa wamepata mafundi wazuri.
Kwa item namba 1 kwa Dar gharama zilikua zinafika hadi 10M kuibadili kichwa cha 6×2 na 4×2 kuwa rigid ya 8×2 na chasis yake pasibo body iliyojengewa na hiyo ilikua mwaka juzi.
Kwa upande wa rigids ambazo unaongezea tu axle moja ya kukata kona yaani item namba 3 hapo juubasi gharama zake hazizidi milion 5.
USHAURI
Kuliko kununua Fuso na kwenda kuifanya tandam aisee ni mara mia uchukue kichwa cha milion 70 ama 80 ukaja kukifanya kiwe kipisi kwa gharama ya juu yake kama M 15 hadi 20 kwa sababu zifuatazo:
😐mende inabeba tani 21(japo kama upiti mzani unaweza kujitwisha hadi tani 25 lakini tandam inabeba tani 17 Maxmum.
😐Mende inadumu na kuvumilia katika suala la engine lakin tandam ni kawaida kuua engine ama kufanya overhaul ikizidi miaka 5 basi una bahati.
😐mende inajitahidi katika suala la breki wakati wa dharula lakini tandam aisee i kudra za Mungu na kujua hili tafuta ajali nyingi za kujaa nyuma kati ya tandam na mende utaniambia.
😐Maboresho ya mende hayaathiri kivyovyote utendajikazi wa engine yake kwani ipo disigned kuhandle hiyo mizigo maana mende nyingi unazikuta zikiwa na HP 300 and plus lakin tandam engine ni 200 HP ikiwa designed kuhandle mizigo ama kutoa nguvu ya kati hivyo kuifanyisha kazi ya kuitwisha tani 17 ni kuiteza engine na ndio maana leakage na kufa ni kawaida.
😐Gharama za maboresh ya kichwa cha scania 4×2 kuwa mende ni karibu sawa na maboresho ya fuso kuw tandam maana Fuso tandam iliyosimama ni kama 80-100M lakini kununua scania 6×2 ama 4×2 P 380 kalii ni mil 70-90 ukiongeza nagharama za maboresho hufika jumla ya 110M kwa mende iliyotayari kwa ajili ya kazi.
Huo ndio ufahamu wangu japo kama kuna wengine wenye ufahamu na data zaidi wanaweza kukuongezea taarifa.