Nahitaji gari used Landcruiser

Nahitaji gari used Landcruiser

Mawio

Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
54
Reaction score
23
Wakuu, salaam!!!..

Ninahitaji used Landcruiser Hardtop, Pickup, Station wagon au Van, iwe na engine ya 1Hz, (engine tofauti na 1Hz tunaweza angalia uwezekano wa mazungumzo pia), iwe katika hali nzuri.

Mwenye nayo ani-cheki inbox au kwa namba hii +255788246790

Bajeti/Pesa niliyonayo mkononi ni Millioni tano kamili (5,000,000/=) Pesa za Ki-Tanzania.

Kama una bodi pekee pia tunaweza angalia uwezekano wa mazungumzo.

Niwatakie kheri ya msimu wa sikuu za mwisho wa mwaka!!!..

Shukrani.
 
Eti 5mil?

Kuna msela humu jf hua ana gari kwa nyuma imeningia vi-pumbu viwili anaweza akauuzia kwa hio bei boss.
 
Kwa pesa hiyo Labda ununue suzuki carry

Ha ha ha ha ha ha ha ha!!!..

Mkuu BONGOLALA!!!..

Used Suzuki Carry ya mkononi ni Millioni 3 Boss, kama unahitaji niambie nikuuzie ya kwangu Mkuu!!!..

Cheers,

🙂🙂!!!...
 
Eti 5mil?

Kuna msela humu jf hua ana gari kwa nyuma imeningia vi-pumbu viwili anaweza akauuzia kwa hio bei boss.

Ha ha ha ha ha ha ha ha!!!..

Mkuu mng'ato kuna siku hio nayo itahitajika nitamtafuta Mkuu!!!..

LOL,

😀😀😀..
 
Yani kwa mbwembwe ulizokuja nazo humu nikajua walau una hata million 40 tu ya kulia lia. We unataka hardtop kwa million 5 labda iwe Land Cruiser ya plastic toy kama yale ya watoto kuchezea. Hio hela hata Engine pekeyake huuziwi
 
Mkuu Maringeni.

Maishani kwepa sana ku-judge watu, "it will save you a day if not a face one day"!!!..

USHAURI WA BURE TU MKUU!!!..

Shukrani.

🙂🙂!!!..
Unadharau vya wenzio.
 
Tuko pamoja Mkuu!!!..

Nikutakie yote yaliyo kheir kuelekea mwisho wa mwaka Mkuu!!!..

Shukrani,

🙂🙂!!!..
Shukrani sana mkuu,Mungu akupe hitaji la moyo wako.
 
Yani kwa mbwembwe ulizokuja nazo humu nikajua walau una hata million 40 tu ya kulia lia. We unataka hardtop kwa million 5 labda iwe Land Cruiser ya plastic toy kama yale ya watoto kuchezea. Hio hela hata Engine pekeyake huuziwi

Mkuu Extrovert!!!..

Salaam.

Mie hupenda sana kuuachia muda ndio useme Mkuu.

Natambua kuna Landcruiser za Millioni 180, 100, 50, 10, 5, n.k inategemeana tu factors kadhaa kama hali ya chombo chenyewe (kipya, kimetumika, kimetumika sana n.k) pia muda (kwa maana ya opportunity cost, exchange value n.k).

Hebu tuuachie muda ndio useme kama hili linawezekana au haliwezekani, mie ninachokuahidi tu ni kuwa nitatuma picha hapa kwa faida yetu sote kama watumiaji wa Jamii Forums ndani ya "UTANDAWAZI NA NGUVU YA MAWASILIANO" Mkuu.

Nikutakie kila lililo la kheir kuelekea mwisho wa mwaka na uingiapo 2019

Shukrani Mkuu,

Sawa mkuu nasubiri mrejesho kabla ya mwaka kuisha
 
1hz mil 22,hiyo hela hainunui hata body
 
Unadharau vya wenzio.

Mkuu Maringeni.

Sijawahi kuwa na dharau na binadamu mwenzangu wala kitu chake hata siku moja, sababu najua wote tulizaliwa tukiwa uchi na hakika uchi tutarudi mavumbini, tukutanayo duniani yote ni ubatili na kujilisha upepo kama alivyopata kunene Suleimani mwana wa Daudi wakati flani.

Wacha nishiriki na wewe kisa changu kifupi, "Mwaka huu January nimeuza gari yangu aina ya Toyota Noah SR40, number D niliyoiingiza moja kwa moja toka Japan, nimeitumia chini ya mwaka mmoja, service ontime e.t.c kwa Millioni tano na laki tano, hii gari ilinigharimu zaidi ya Millioni kumi na moja na laki mbili baada ya kuilipia ushuru mpaka kuiondosha bandarini, lakini kwa dharura niliyoipata ya uhitaji wa pesa hio Millioni tano na laki tano ilikuwa kama muujiza kuipata na nashukuru niliweza kutatua shida yangu bila kuharibu mambo mengine makubwa zaidi"!!!..

Nimejifunza kuto-judge mahitaji wala hali (situation) za watu, wakati mimi au wewe unaweza kuwa unaidharau millioni tano, kuna mtu hapa duniani millioni hio tano ni mwanga na ukombozi wake kwa hali anayoweza kuwa anakumbana nayo na ikawa ina maana kuliko gari chakavu aliyopaki uwani.

Hebu tukwepe ku-judge hali za watu na tuachie fursa ya jukwaa hili kuwaunganisha watu kwa madhumuni mbalimbali na kutokana na mahitaji yao ipate nafasi stahiki.

Nitangulize shukrani na kukutakia salama na kila lililo kheir kuelekea mwisho wa mwaka huu na unapoingia mwaka 2019.

Shukrani sana Mkuu..

¬Mawio 🙂🙂!!!..
 
Sawa mkuu nasubiri mrejesho kabla ya mwaka kuisha

Akhsante Mkuu.

Ni tegemeo langu kuwa nitakuwa na mrejesho kabla ya wakati huo au kwa namna vile muda utakavyoamua kupeleka mambo Mkuu!!!..

Tuko pamoja ndugu yangu.

Shukrani,

¬Mawio 🙂🙂!!!..
 
Back
Top Bottom