Hapa JF kuna matatizo kadhaa yanayojirudia karibu kila siku kwa watu wengi, matatizo haya yanaonesha udhaifu wa elimu Tanzania.
1. Watu kushindwa kufikiri kidhahania (abstract thinking). Mada inaweza kuwa na maana sana in the abstract, wao wanaondoka kwenye abstract topic wanakuja kwenye actual.
2. Watu kuacha kujadili mada ya msingi na kujadili mfano uliotolewa katika mada. Umetoa namba ya Sh 500m. Watu wameshindwa kuichukulia namba hiyo kama mfano na kufanya abstract exercise ya biashara kubwa kwenye hiyo range/tax bracket. Wameifanya hiyo namba kuwa ndiyo topic.
3. Watu kufanya logical fallacies, mfano, kuacha kujadili mada, na kumjadili mtoa mada (ad hominem attack). Wameshindwa hata kushauri kwa caveat "if at all this is legit...". Tanzania tunaenda na "guilty until proven innocent" instead of "innocent until proven guilty".
Nilimueleza mtu hapo juu kwamba kama unayo hiyo hela au huna si kitu muhimu, kitu muhimu ni hoja uliyoianzisha kuwa, ukiwa na hiyo pesa unaweza vipi kupata ushauri kuhusu jinsi ya kuiwekeza?
Tatzo la wabongo, Wanasema watu wenye pesa hawapo JF na hawatumii social networks,
Hii ni tabia ya maskin wote huwa tunatabia ya kuamini kuwa tukiwa katika kund hata kama hatujuani tunaamini wote tuko sawa, hii kitu watu wazembe kifkra na kiutaftaji huitumia kama njia pekee ya kuwapa matumaini ya kuamini kuwa wote tunafanana na wote tuna shida moja so ikitokea mtu akajitambulisha kuwa sio mwenzao hapo ndioo vita, ugomvi, na chuki huanzia,
Suala la mtu kuwa sio mfuasi wa mitandao ya kijamii ni hulka ya mtu wala sio pesa, ninao watu maarufu wengi na matajiri wengi ninaojua wapo mitandaoni na tunabishana nao humu maana tajiri ni binadam mwenye hisia na hulka za kibinadam pia,
Kuna watu hawana pesa na hawana mda na mitandao suala hili lipo kihulka tu wala sio kifedha.
Vijana wajinga huamini Milionaire na Bilionaires hawapati mda wa kutumia mitandao ya kijamii wapo bize kutafta pesa mda wote wchich is standard Idiot, kama bodaboda ambae mda wote yupo road lakin bado anapata mda wa kupita mitandaoni, mama muuza genge nae anapata mda wa kuingia mtandaoni, mangi muuza duka nae anapata mda wa kuingia mtandaoni, ni ubize gani huo ambao bilionaire anao ambao hapati mda wa kuingia mtandaoni???
Hakuna tajiri aliebize kama maskini walivyobize tajiri yeyote pesa ina run kwenye mifumo wala sio kutumia pysical excise kupata pesa, matajiri wengi wanashinda mitandaoni kusoma coment na kupost content labda matajiri wasiofanya hivyo ni wale matajiri wa vijijini wafugaji na wazee wa mikoani, ila most highlighted people wanamiliki account fake zaid ya 10 na wanakuwa active nazo issue siriaz wanaziona na mizaha pia wanaiona na kuchangia,
Nina refference kuna staa mmoja ni mkubwa sana tz hapa na ni ndugu yangu ninajua anamiliki account fake anazotumia kusocialize na watu ila linapokuja suala la msingi ndio hutumia official page yake,
Pia nina rafiki yangu ambae mzee wake ni kiongozi mkubwa sana Tz ila jamaa alishawahi kuchukua sim ya mzee wake na akaona app ya Fb ile kuifungua tu akakuta jina sio lake na kuchek kwenye activity log kakuta mzee yuko kwenye conversation kibao za utan na ujinga kibao anacoment na kulike pia,
So watu wengi wenye pesa wanahofia kutumia Ig halisi sababu wapo kwenye spotligh ila hulka za kibinadam hazijawahi kubadilishwa na pesa hata kidogo,
Hata hapahapa JF naamini wapo mabilionaire kibao na tayari nimekutana na watu ninaohitaji na nipo kwenye hatua nzuri ya kutimiza hitaji langu ko wewe kama unaamini JF kila mtu yupo hapa kwa OFa ya MBS za tigo za bure, endelea kuamini katika imani yako,
Pia msaada kukutana na kundi la watu unaoamini mnafanana matatizo haisaidii kupunguza tatzo lako wala haiongozi chochote kwako. Ili ufanikiwe amini ulizaliwa peke yako, amini utakufa peke ako, amini mzigo uliobeba umeubeba peke yako na utautua peke yako, acha kutafta campany kwenye shida zako haitakusaidia, kujua maskini mpo wengi haipunguzi umaskini wako, ila ukijua wewe ni maskini peke yako itakusaidia kupambania ndoto zako na kuepuka umaskini,
Watu wengi huamini msiba wa wengi hauna kilio ila cha kujua hapa ni kwamba haibadilishi uhalisia wa kifo kifo kitakuwepo palepale na utakuwa umekufa hata kama hakuna kilio hakuna kinachoongezeka kwako.
Ko jitahidi kupokea shida zako wewe kama wew, usiamini kaka wote tulioko huku tunafanana maisha.