Mtoa mada katika kitu usifanye ni kutrade in simu yako. Nina mfano (kisa):
Nilikua na iPhone 8 nimenunua duka flani Makumbusho na risiti/wallanty yao ninayo. Waliniuzia 550. Baada ya miezi 6 hivi nikarudi kwao nikataka nitrade wanipe iPhone 11. Wakaicheki wakasema niongeze Laki 9 nipate GB64 nikauliza kwani nikisema nitoe cash bei gani wakasema Mil 1.05 (Mil 1 na elfu 50).
Kwahiyo wameivalue kwa Tsh laki 1.5 simu yangu.
Nikisema nitakuja. Nikatafuta namba nyingine nikawapigia nikasema nataka simu, used, iPhone 8 nyeusi GB64 (kama yangu) wakasema ipo used best condition BH96% kwa Laki 4 mwisho kabisa 350k.
Nikasema nakuja dukani. Dakika 10 mbele wakanipigia kwenye ile namba nyingine ambayo nilipiga ninavoenda kutradein wakasema vipi kuhusu tradein? Kama vipi njoo tuinunue simu yako (i8) hafu wewe utakua unalipa kidogo kidogo iyo laki 9.
Hitimisho: Niliamuaga tu kununua iPhone 11 hafu ile 8 nikampa dogo.
Yaani tradein ni biashara ya kifala haijawahi tokea