Nahitaji kazi/ ajira

Nahitaji kazi/ ajira

juzeyr

New Member
Joined
Oct 5, 2024
Posts
1
Reaction score
9
Habari za wakati huu.

Majina yangu ni XX ni msichana wa miaka 25 ninaishi temeke Dar es salaam. Mimi ni mhitimu wa elimu ya chuo kikuu mwaka 2022 katika kituo kilichokuwa kinaitwa “TANZANIA-MOZAMBIQUE CENTRE FOR FOREIGN RELATIONS” lakini kwa sasa kinaitwa “ DR. SALIM AHMED CENTRE FOR FOREIGN RELATIONS” kilichopo kurasini, Dar es salaam.

Nimehitimu shahada ( Degree) ya Mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia yaani “INTERNATIONAL RELATIONS AND DIPLOMACY’ na kupata ufaulu wa GPA( 4.3) daraja la juu la kati yaani (UPPER SECOND CLASS), pamoja na hilo ninaumahiri mkubwa wa kuzungumza, kusoma na kuandika lugha ya kingereza na kiarabu kwa ufasaha.

Pia nina ujuzi wa kiendaji ambapo nimepata mafunzo ya vitendo( field practice) kupitia taasisi mbali mbali zikiwemo NSSF, JNICC, Legal and Human Rights Center na Chuo cha Diplomasia kwa ujumla ambapo vimenijengea uwezo wa kitaaluma na uzoefu katika nyanja tofauti tofauti za uwajibikaji.

Katika muda wangu wa ziada napendelea zaidi kuchambua na kufatilia habari mbali mbali, kusoma vitabu, kutoa nasaha na kuhamasisha.

Mapendekezo yangu ningependa kazi yoyote hata ambazo zipo nje ya taaluma yangu ili nipate uzoefu zaidi zilizopo mkoa wa Dar es Salaam zaidi lakini hata ikitokea nje ya mkoa husika nipo tayari kwa hilo.

Ahsanteni sana
 
Mungu akutangulie .. maelezo yako yamenyooka mno
 
Umejitahidi sana kujielezea vizuri. Nakuombea ufanikiwe vizuri
 
Back
Top Bottom