Nahitaji kazi yoyote, nipo Morogoro

Nahitaji kazi yoyote, nipo Morogoro

Siyoi4

Member
Joined
May 26, 2021
Posts
5
Reaction score
3
Habari wakuu,

Nahitaji kazi yoyote kwa sasa, kiwango cha elimu yangu ni shahada ya ualimu.

Ila nipo tayari kufanya kazi yoyote nipo Morogoro maeneo ya Oil Com.
 
Ingekuwa umesomea fani ya Afya leo hii ungepata Kazi.
Kwa fani yako ya Ualimu jaribu kutafuta kwenye Shule Binafsi hizi za English medium, ukikosa waombe wakupe nafasi ya kujitolea wakiona juhudi zako watakuchukua jumla.
 
A

Ahsante
 
Mkuu umejalibu kumuona Abood?
Hapana mkuu japo nimezunguka viwandani kule ila wananiambia nafasi zitatoka kuanzia mwezi wa 8 hivyo. Ndiyo maana naendelea kutafuta popote.
 
Habari wakuu,

Nahitaji kazi yoyote kwa sasa, kiwango cha elimu yangu ni shahada ya ualimu.

Ila nipo tayari kufanya kazi yoyote nipo Morogoro maeneo ya Oil Com.
Mungu akufanyie wepesi!! Ila ukipata kazi yoyote ipende na kuiheshimu!! Maana watoto wetu mliosoma ukipata kazi yoyote kama ulivyosema, usomi unawaathiri sana!! Kuna jamaa mmoja alimpata msomi, alipofika kazini kutwa kulalamika na wafanyakazi wenzie kuwa yeye ni msomi bosi anampa kazi za wasiosoma!!
 
Nashukuru sana kwa sala na pia ushauri mzuri ulionipa. Ni kweli baadhi ya sisi vijana tumejisahau, tunautumia usomi wetu vibaya kujikweza kwa wengine kwa kuona hatuna hadhi ya kufanya kazi fulani.
 
Back
Top Bottom