Ndugu zangu ninaomba kujuzwa kwa wale wazoefu wa biashara ya kwenda Mombasa kufuata vijora ni taratibu zipi natakiwa kuzifuata na mtaji ama kianzio cha biashara na tax pia wanatozaje, naombeni michango yenu na nataguliza shukrani za dhati kwenu.
Kabla hujaenda huko Mombasa Bora uingie chimbo apo apo Kariakoo, waombe namba za wanaoshona vijora huko Mombasa ukipata namba zao unakua unanunua wanakutumia kwa Basi kuliko wewe kwenda ni gharama na vijora ukienda hupati faida.