Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dar es salaamUko mkoa gani.
Miundombinu ikiwa vizuri faida ipoHata mm naifikiria siku moja ntakuja kuifanya
Wazo zuli, lakini maharage yana aina tofauti tofauti lazima uangalie unataka kuuza maharage ya aina Gani? Na utaka kuuza kwa level ipi?? Jumla au reja rejaNatumai mko vema nilikuwa nahitaji kuanza biashara ya maharage mwenye uzoefu wa masoko na changamoto zake.
Mwenye uzoefu karibu.
Mwaka huu kwa katavi yaliishia debe Tsh. 60000/=Maharage yanalipa mkuu hasa ukipata chimbo zuri la kujumlia na kuuzia,mikoani maharage kununua kipindi cha mavuno mwezi April na May debe Tsh. 30,000 - 35,000 lakini kipindi cha OCT,NOV na DEC huku huku mikoani yanauzwa kwa Tsh. 60,000 - 70,000 tena yanatafutwa kwa torch,so unaweza pata faida pasipo gharama ya kusafirisha kikubwa uvumilivu na kuuacha mzigo store. Mimi binafsi nimeyalima takribani ekari nne matarajio ya mavuno ni takribani gunia 16 na kuendelea na mrejesho wa faida ni miezi hiyo tajwa. Usighairi huo mpango utakuja kutushukuru,maharage dili kuliko mahindi changamkia hiyo fursa.