Maharage yanalipa mkuu hasa ukipata chimbo zuri la kujumlia na kuuzia,mikoani maharage kununua kipindi cha mavuno mwezi April na May debe Tsh. 30,000 - 35,000 lakini kipindi cha OCT,NOV na DEC huku huku mikoani yanauzwa kwa Tsh. 60,000 - 70,000 tena yanatafutwa kwa torch,so unaweza pata faida pasipo gharama ya kusafirisha kikubwa uvumilivu na kuuacha mzigo store. Mimi binafsi nimeyalima takribani ekari nne matarajio ya mavuno ni takribani gunia 16 na kuendelea na mrejesho wa faida ni miezi hiyo tajwa. Usighairi huo mpango utakuja kutushukuru,maharage dili kuliko mahindi changamkia hiyo fursa.