Nahitaji kuanzisha gazeti very soon, kuna maujanja nataka nipate kutoka kwenu

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Posts
2,149
Reaction score
1,718
Kama mada inavyosema hapo juu, nna wazo hilo na kuonesha nimedhamiria tayari nimeandaa business plan yangu. But ili plan iwe real sina budi niwe na data ambazo ni real. Kwa mtu mzoefu na mambo ya magazeti na takwimu angeweza kunisaidia nijue wastani wa watanzania wanaosoma magazeti kila wiki moja. Ningefurahi kama ningepata taarifa za kitakwimu zaidi yaani kati ya watanzania 1000 ntapata wasomaji wangapi?

Najua kuna watu wanafanya kazi global publishers, mwananchi comm na ipp media ningepanda wanipe hata estimation ya magazeti ambayo wanayaproduce kwa kila toleo moja ili na mimi niweze kufanya estimation vizuri.

Nimedhamiria sana kwa hili japo sina cash mfukoni am not bothered maana najua kama if this idea work out no investor can turn it out. Ila kwanza nataka niwe done with the plan.. Yaani ni explore kila kitu from the scratch mpaka gazeti litapoingia sokoni, then ndo nijue zinahitajika kiasi gani cha pesa na mipango ya kutafuta capital ndo ianzie hapo.

Naombeni huo msaada sana, nna mawazo mengi sana. Lakini kama mjuavyo vision without excecution is halucination. Sasa ndo hivyo mi nshachafukwa na roho i dont want either of my ideas to become halucination. I have guts now to start from the scratch and face any monster, failure not an option.

2015- think big, hustle hard, get started, sense of urgency, failure not an option, get rich or whatever, clock is ticking.

Jamani msione nna maneno mengi ila ndo hivo tu, vijana tushachafukwa na roho.
 
unachotakiwa kujua gharama za kuprint je litakuwa linatoka kwa muda gani

je utasambaza Tz yote

je la udaku au?

waandishi?

cash lazima uwe nayo
 
mwenye kujua kwanza gharama za kuprint angekuja kutwambia
 
Mengi hadi leo kashindwa kulipa waandishi Ingawa eti ni milionea. Rostam Aziz vile, vile. Sasa Mbowe ndio kabisaaa. Kwa nini usianzishe blog tu?
 
unachotakiwa kujua gharama za kuprint je litakuwa linatoka kwa muda gani

je utasambaza Tz yote

je la udaku au?

waandishi?

cash lazima uwe nayo
Hayo yote nimeshayapanga sasahiv natafuta baadhi ya clue kama gharama za kuprint. Issue ya distribution haitanisumbua maana nimeshaset model ya kuyadistribute ambayo ni ya uhakika. Suala ambalo bado sijalisolve ni kwenye production hasa hasa printing and getting paper material ambayo suitable. Kuhusu man power hilo sina wasiwasi nalo kabisa wapo wengi sana.
 
Mengi hadi leo kashindwa kulipa waandishi Ingawa eti ni milionea. Rostam Aziz vile, vile. Sasa Mbowe ndio kabisaaa. Kwa nini usianzishe blog tu?
Wao ni wao na kushindwa kwao hakumaanishi kila mtu atashindwa. May be they dont take it as a business but just political weapon. Kwahiyo kama ni hivo lazima utegemee watashindwa kama unavyo maanisha wewe ingawa binafsi sijui kama ni kweli wameshindwa. Halafu unaposema Mengi mpaka leo kashindwa kuwalipa wafanyakazi wake unamaanisha nini? Hivi unajua kwenye mambo ya uchumi kuna kitu kinaitwa labour productivity theory, waweza kuwa bilionea lakini ikiwa moja kati ya biashara zako sio productive, how could you pay your factors of production? We unafikir bakhresa akianza kupata hasara (siombi litokee) unategemea nini, automatically watu wataanza kufukuzwa kazi maana there would be know source of paying them. Kwa hiyo ikitokea hivo utasema bahkresa ni tajiri lakini anashindwa kulipa mishahara. Aisee broh saa nyingine tujenge logic na tunayoyasikia na saa nyingine lazima tuwe different.
 

Kila la heri na hiyo logic ambayo hao wote wameshindwa kuiona
 
Idea iko poa and i wish you all the best..Lakini ukifuatilia global trends, utaona kwamba biashara ya magazeti inaanza ku decline na countries kama USA isha predict biashara ya gazeti itakufa nchini humo by 2020. so make sure una draft innovative bussiness model since utakua unapambana na technology pia
 


biashara ya magazeti kamwe haiwezi kufa,pamoja na kuwa kila kitu computer sasa marekani,ata watoto wadogo kabisa miaka 2 wana ipad lakin magazeti bado yanasomwa sana,na wafanyabiashara wengi wanatangaza matangazo yao.

nasoma hivyo kwa uzoefu wangu na uko USA ndio nilipo
 

Offcourse magazeti ni a big part of the society & from that point of view ni ngumu kuona yana kufa..They are part of our culture.

Lakini from a bussiness perspective ni ngumu kuona yaki survive since tayari yameshapoteza half of its classified advertising to the internet..na magazeti mengi yana depend at around 70% on classified advertisement..

But only time can tell..
 

na mtandao kumejaa kila mtu ana blog
 
Unataka kutoa gazeti la kila siku, kila wiki au kila mwezi? Hilo ni swali la kwanza unatakiwa kujiuliza. Pili, unataka kusajili gazeti au unataka kununua linalomilikiwa na mtu.
Pia, ujue unataka kutoa gazeti la mlengo upi? Siasa, dini, michezo, afya au udaku? Ukijijibu haya maswali omba kuonana na mmiliki au mwendeshaji wa gazeti la mlengo kama wa gazeti utakalo ili akusadie maelekezo.
Kwa kifupi gazeti ni moja ya biashara zinazohitaji umakini na kufanyia utafiti wa kutosha, kwa sababu ina Uwezo wa kukutia hasara hata ya milioni hamsini kwa mwezi mmoja tu.
Usiyaone yanatoka tu ukadharau hadi ukahisi ni biashara rahisi tu ambayo unaweza kuifanya kama kufungua bar au restaurant.
Unapaswa kuomba ushauri kwa wamiliki wa magazeti sio waandishi wa habari, kwani wao taaluma yao ni kuandika habari na kumiliki gazeti ni biashara.
Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…