Nahitaji kuanzisha gazeti very soon, kuna maujanja nataka nipate kutoka kwenu

Mengi hadi leo kashindwa kulipa waandishi Ingawa eti ni milionea. Rostam Aziz vile, vile. Sasa Mbowe ndio kabisaaa. Kwa nini usianzishe blog tu?

Kila siku duniani ikiwemo tanzania kuna baadhi ya biashara nyingi tu zinafungwa au kufilisika kwasababu mbalimbali, na kila siku biashara mpya zinazofanana moja kwa moja na zilizofungwa zinafunguliwa. Kufu kwa biashara sio kigezo chakutofanya biashara bali ni moja ya njia nzuri zaidi ya kujifunza kwann kashindwa
 
mkuu umemaliza watu wanaona mtu anasomagazeti kwa mia tano au 800 wanadhani gazeti lele mama
 

Nenda Idara Ya Habari Na Maelezo Mtafute Binti Mmoja Wa Kihaya Anaitwa Johari Kachwamba Atakusaidia.
 
Mengi hadi leo kashindwa kulipa waandishi Ingawa eti ni milionea. Rostam Aziz vile, vile. Sasa Mbowe ndio kabisaaa. Kwa nini usianzishe blog tu?
Ni point nzuri ya kuifikiria. Lakini nani ana hela zaidi, mtu kama Kubenea au hao heavyweights kina Mengi, Rostam, na Mbowe?

Manake naona Kubenea anafungiwa leo asubuhi kesho usiku anaibuka na gazeti lingine. Na sio Kubenea tu, kuna magazeti kibao yameanzishwa miaka ya karibuni, Jamhuri mfano, matajiri gani wanalimiliki na je wana hela kuliko kina Mengi na Rostam? Kuna magazeti ya misikiti, makanisa n.k. ambao sidhani wana hela kama IPP Media au conglomerate la Rostam. By the way, Rostam tumtoe, kwa saab nadhani at some point aliamua ku shed some of his businesses, kama share za Voda aliuza, inavyoaminika, lakina haina maana biashara ya simu ilimshinda. Na labda magazeti hayakumshinda. Again, kama Kubenea anaweza. Unasemaje?
 
ushauri wangu ajiri editor wengine wote walipe kadri wanavyoleta story vinginevyo utakuwa na mzigo wa kulipa watu wengi lakini hawana mchango mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…