Nahitaji kubobea kwenye uvuvi

MUTTAZ

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2016
Posts
296
Reaction score
237
Jamani habari za leo!

Naomba kupata uzoefu wa uvuvi wa samaki hasa Sangara ziwa Victoria, nahitaji kuanza kuvua samaki hao ila sina uzoefu juu ya gharama za kumiliki mtumbwi, bei ya nyavu au migonzo kama ninavyosikia ikiitwa na kipato kitakachopatikana.

Nimeona nije hapa nipate uzoefu kwa wale wanaojua au wenye ujuzi wa hili tafdhali.

Karibuni wavuvi wenzangu!
 
Mkuu we upo wapi kwa sasa.? ila nakushauri ni nora ukajisogeza taratibu mwaloni ukapate hizo taarifa kwa usahihi.
 
Achana na nyavu mkuu utafirisika kabisa nakushauri mgonzo angalau kwani unatumia Mtaji kidogo.
 
Naomba kufahamu chambo nzuri kwa kuvulia kambale
 
Andaa 250,00/= ya vifaa vyake kisha ili uvuvi wako uende vema unapaswa kuwa na mtumbwi wako mwenyewe. Unaweza kununua kwa mtu bei kuanzia 200,000/= ila mtumbwi mpya ni 300,000/= inshort unatakiwa kuandaa kama laki 5 hivi na msimu huu ndiyo wenyewe.

Ukibahatika kutega vizuri hiyo pesa inarudi ndani ya wiki tu unaanza kula faida. Kama upo serious tunaweza kuwasiliana
 
Ndugu nami nimetokea hapo Dar miaka ya 1990, baada ya kumaliza elimu ya sekondali.kuna shugh'uli nyingi nilizipitia, ila kwa ufupi hii kazi ya uvuvi is the best: nimepata uzoefu mkubwa tu na kwa sasa Alhamdullillah naridhika na nilivyovuna kutokana na kazi hii. Nakukaribisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…