Nahitaji kufahamu juu ya masuala ya hisa (share)

Nahitaji kufahamu juu ya masuala ya hisa (share)

The Ideologist

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2012
Posts
486
Reaction score
256
Kwa yoyote Mwenye ufahamu juu ya biashara ya hisa faida, hasara zake Maana nataka kuwekeza uko?

naamini wataalam watanisaidia kwenye hili mfano hisa (share) CRDB, NMB, TWIGA NA kampuni yoyote kubwa ambao naweza kupata faida
 
Aisee, kuna rafiki yangu last week tulikua tunaongelea hii kitu. Kuna mtu anafanya training ya hizi makitu, sasa anachaji per group na fee ilionekana kuwa kubwa bado. Nitumie pm, then nitakutaftia namba ya hao trainers nikupatie ujipange. Wana train na kukupa guide wakati gani wa kuuza ama kununua.
 
thanks utakuwa umenisaidia vya kutosha
 
samahan kwa ukimya ila search on google abt ''hisa in jamiiforums'' na jaribu kusoma hizo thread na utapata maana kamili ya hisa na wher to invest and where not
 
kuwekeza kwenye hisa ni kuzuri zaidi na kuna lipa zaidi, ukinunua hisa mwishoni mwa mwaka unapata gawio kutegemeana na faida iliyotengenezwa na company.

Hizi hisa zipo za aina tofautitofauti ,kuna common stock na preffered stok,.Ni PM ili nikuelekeze vizuri
 
Kwa yoyote Mwenye ufahamu juu ya biashara ya hisa faida, hasara zake Maana nataka kuwekeza uko?

naamini wataalam watanisaidia kwenye hili mfano hisa (share) CRDB, NMB, TWIGA NA kampuni yoyote kubwa ambao naweza kupata faida

kuna kuwekeza kwa muda mrefu (yaani miaka 5 na kuendelea) au kufanya biashara ya kuuza na kununua kutegemea upandaji na ushukaji wa bei za hisa.

binafsi naamini katika kuwekeza kwa muda mrefu yaani kununua hisa na kungojea kwa muda mrefu. japokuwa hii inataka moyo hususan bei za hisa inapoporomoka na kufika chini ya bei uliyonunua. wapo wengine wao wanajaribu "kuliotea soko" yaani kuuza na kununua kutegemea anahisi bei zinaelekea wapi.

kwa shule ya haraka haraka kuhusu biashara ya hisa (hiyo fool kwenye link isikukatishe tamaa) hebu pitia website hii Fool.com: Stock Investing Advice | Stock Research
 
hisa ni vipande vya mtaji wa kampuni vinavyotolewa sokoni ili watu wanunue.

badala ya kampuni kumilikiwa na mtu mmoja, inapeleka sehemu ya umiliki kwa watu wengine.

kwa mfano, kampuni X, ya Mr. J yenye mtaji Bilioni Tano na Hisa 3,000 anaamua kuorodhesha kampuni yake lets say hisa 1,500 ili awauzie watu kwa kila hisa kwa bei fulani....

ukinunua hisa faida zake ni
1. unaweza kuuza muda wowote ukihitaji pesa
2. unaweza kuuza kwa faida, mf. umenunua hisa za NMB mwezi huu kwa sh 300, bei zkipanda baada ya miez mitatu unaweza kujikuta unauza sh.400
3. unaaweza kupata gawiwo la faida ya kampuni husika (japo, sio lazma kampuni ilipe gawiwo, yaan dividend)

4. unaweza kumrithisha mtu yeyote (mwanao)
5. unaweza kukopea pesa benki ukitumia kama amana, kama.inavyokuwa nyumba!!

......sorry nilikuwa usingizn hapa, ndo maana nimeandika kwa haraka!!!!! kama kuna anayehitaj maelezo zaidi, niulizeni!!!!

PJN
MBA Finance
 
kuna kuwekeza kwa muda mrefu (yaani miaka 5 na kuendelea) au kufanya biashara ya kuuza na kununua kutegemea upandaji na ushukaji wa bei za hisa.

binafsi naamini katika kuwekeza kwa muda mrefu yaani kununua hisa na kungojea kwa muda mrefu. japokuwa hii inataka moyo hususan bei za hisa inapoporomoka na kufika chini ya bei uliyonunua. wapo wengine wao wanajaribu "kuliotea soko" yaani kuuza na kununua kutegemea anahisi bei zinaelekea wapi.

kwa shule ya haraka haraka kuhusu biashara ya hisa (hiyo fool kwenye link isikukatishe tamaa) hebu pitia website hii Fool.com: Stock Investing Advice | Stock Research

mmmh,
hisa (share) hawawakezi jamani,
labda unachanganya na bonds.....

Bonds ni miamala ya fedha inayotumiwa na serikali au kampuni kupata pesa, na inakuwa ya miaka 5, 7 hadi 10.

mfano NMB inaweza ku-issue bonds kwa makampuni mengine lets say ya sh bilion 5 kwa muda wa miaka 7, kwa malipo ya sh 8 bilioni ikiiva na CRDB akanunua.......

likewise,serikali ndio muhusika mkubwa wa hii biashara ya bonds, ikikwama hupata pesa ya haraka kwa kuuza bonds kwa taasisi za fedha kama benk na kampuni zingine....

hapana sijachanganya na bonds. nazungumzia hisa (shares).
labda tunaliangalia tofauti neno kuwekeza (investment).

mimi nanunua hisa kwa ajili ya kuwekeza yaani sitarajii kuziuza kwa muda mrefu labda kampuni ipate matatizo makubwa. kushuka wala kupanda bei za hisa nilizonazo haziniongozi katika maamuzi yangu ya kuuza hisa zangu (hapa pia inategemea mkakati wa mtu na mtu).

binafsi naamini kuuza hisa ulizonazo kwa kuwa tu bei ya hisa imepanda ni kuwanufaisha mabroker kuliko wewe mwenye hisa. na mtu anae uza na kununua hisa kwa msukumo wa bei za hisa tu huyo kweli sio mwekezaji bali ni "trader".
 
Back
Top Bottom