Nahitaji kufahamu procedure za duka la pembejeo na mifugo (kilimo na mifugo)

Nahitaji kufahamu procedure za duka la pembejeo na mifugo (kilimo na mifugo)

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Wakuu kheri nyingi kwenu. Happy Sunday!!

Nimevutiwa sana na biashara ya duka la kilimo na mifugo lakini kwakweli sijui vigezo ambavyo napaswa niwe navyo ili nifungue duka hilo na changamoto zake pia.

Hivyo nilikuwa naomba sana kwa wenye uzoefu na hii biashara wanipe ABC za kuanzia na pia mtaji mzuri ni upi naweza kuanza nao na sehemu nzuri ya kuchukulia bidhaa zote(bei nzuri)

Nahitaji kujua hayo na mengine mengi ambayo siyajui kama ni dawa Gani shart sipaswi kuzikosa dukani nk!

Ahsante sana waungwana.

#Niko Porini Niko site kwa wagumu tu
Manyanza
PXL_20260621_075152691.jpg
 
Unatakiwa upate wataalamu wawili wa kilimo na wa mifugo wenye vyeti na leseni
 
na mtaji wa kueleweka, location na uwe na good supplier
 
Nikuulize swali maana hizi mambo nimefanya sana ila nilisimama kidogo .
1. Uko duka unakoweka wanalima misimu yote kiangazi na masika
KWa ufupi inabidi ukauzulie mafunzo ya THPA hada ilikuwa laki nne na wanazunguka kwa kanda 5 za hapa tanzania na mwisho wa mafunzo kuna mtihani ukifeli upati cheti cha kuuza viuatilifu vyote utasubili hadi mwakani mafunzo uanza mwezi wa sita hadi wa tisa huko.
TFRA wao awana ada utoza pesa kidogo ya kuandaa cheti baada ya kuuzulia mafunzo hii ni upande wa mbolea

Kuhusu mbegu wapo TOSCI
Baada ya kupata hivyo vibali nenda ukafate leseni ya biashara halmashauri uanze kazi mengine utajifunza kulingana na eneo ulipo hii kazi inabidi uwe mdadis kama ujasomea uwe na maneno matamu ya kuwavutia wateja

Ukitaka uongeze dawa za mifugo hapo umtafute mtu aliyesomea mifugo na ana cheti cha balaza la veterinary tz .q
 
vibari vyake unaweza kujikuta mpaka na picha ya raisi ikahusishwa .
 
Back
Top Bottom