Nahitaji kufanya biashara ya vitenge

bkidude

Member
Joined
Jun 22, 2015
Posts
84
Reaction score
21
Nahitaji kufanya biashara ya vitenge toka Congo na Malawi ananyeweza kunipa link ya jinsi ya kupata vitenge huko kuleta Makambako.
 
Ngoja waje wenye uzoefu bila shaka utapata msaada.
 
Vitenge vinavyotokea congo vinapatikana kigoma kwenye maduka ya jumla ya vitenge pale nwanga sokoni. hujasema utaviuza wapi lakini kana ni Dar ni vema UKAWA unasafiri na order kabisa kutoka kwa wafanya biashara wa kariakoo yani ukifikisha mzigo tu basi unautoa, ni biashara nzuri sana
 
Vitenge vya Congo hupatikana sana kigoma na kwa zamani pia Tunduma vilikuepo lakini wamebana sana hivyo kwa urahisi nenda kigoma ambao huvipitisha kwa njia za maji kupitia ziwa Tanganyika bila kodi na waxy original bei ya jumla ni 27 elfu na kuna vitenge vinaitwa Hita Get ambavyo ni vipya huuzwa 24 elfu kwa bei ya jumla na maduka yapo Sehem inaitwa Mwanga ndio kuna maduka ya jumla jumla
 
Namna ya kufika Kigoma Nenda Ubungo tafuta mabasi yanayoitwa SARATOGA ambapo utapanda basi kama leo saa kumi na mbili na kesho yake saa mbili au saa tatu unafika kigoma nauli ni 70 elfu lakini pia unaweza kupanda mabasi mengine kama mvullah, adventure ambayo hupitia Tabora au kahama nauli yake ni 60 elfu lakini haya sio wazuri sana kwani unaweza kufika kigoma kesho yake saa 10 jioni
 
Lakini pia Vitenge vya Malawi hivi hutoka sana Zimbabwe na Msumbiji ndipo huingia Malawi na unaweza kuvipata kwa urahisi maeneo yote ya mipakani na miji kama Muzuzu , Blantaya, Lilongwe na unavushia Boda ya kyela sana sana na wengine huvusha kwa kutumia ziwa Nyasa ili kukwepa kodi na bei zake kwa jumla ni kama 13 elfu hadi 16 elfu ambapo wewe utaviuza kati ya 20 hadi 25 kama sijasahau.
 
Waweza kuuliza swali lingine kama nitaweza nitakujibu ili tuelewashane
 
Jamani namimi nataka kufanya biashara ya rim paper bt natakakuchilia mzgo Nairobi Kenya bt cjui huko katoon moja ya rim paper wanauza sh ngapi, jamani wadau nisaidien kujua
 
Jamani namimi nataka kufanya biashara ya rim paper bt natakakuchilia mzgo Nairobi Kenya bt cjui huko katoon moja ya rim paper wanauza sh ngapi, jamani wadau nisaidien kujua

rim papers kwa Uganda , Kenya na Tanzania zipo juu labda ujaribu kuzitoa Afrika kusini kwenye viwanda au mataifa jirani na Afrika kusini kama Zambia au Zimbabwe na naamini Msumbiji pia zitakua chini kwani wanazitoa SA ambapo ni karibu
 
rim papers kwa Uganda , Kenya na Tanzania zipo juu labda ujaribu kuzitoa Afrika kusini kwenye viwanda au mataifa jirani na Afrika kusini kama Zambia au Zimbabwe na naamini Msumbiji pia zitakua chini kwani wanazitoa SA ambapo ni karibu

Mtaji wangu co mkubwa sana, ningejua kwakenya nishngapi ingenisaidia kidogo coz tayali nishapata soko la uhakika apa arusha..
 
Kwani hakuna supplies wa kufikisha dar? Ni adi uende kigoma pale pale?
 
Na vipi kuhusu watu wa ushuru, hawatasumbua njiani? Maana mara nyingi wanavizia mabasi yanayotoka huko wakijua kuwa lazima kuna wafanyabiashara waliofunga mzigo wa vitenge.
 
Kwani hakuna supplies wa kufikisha dar? Ni adi uende kigoma pale pale?

Ukinunulia Dar watakupiga na ni Rahisi kukutana na feki kibao, ukifuata kigoma mara mbili au mara tatu unajenga wenyeji wako kibiashara halafu wale wauzaji wa Kigoma wataanza kua wanakuagizia Dar kwa mabasi then wewe unapokelea Dar .
 
na vipi kuhusu watu wa ushuru, hawatasumbua njiani? maana mara nyingi wanavizia mabasi yanayotoka huko wakijua kuwa lazima kuna wafanyabiashara waliofunga mzigo wa vitenge...

Unatakiwa uchangamshe akili yako isilale na ujiongeze ili kusongesha mambo kwenye biashara vizuizi vipo lakini ni kukomaa sana na kuhusu bei naamini nitawauliza washkaji zangu wa Nai City wakinijibu nitakueleza usijali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…