Wakuu elimu yangu ni kidato cha nne,division (iii)ninania ya kusomea IT,kwa njia ya mtandao(on line)kutokana na nafasi yangu kuwa ndogo kuhudhuria darasani,je nichuo gani ninaweza kujiunga nacho ambacho kinatambulika na serikali.Nadhani ni vema nianze na diploma...!!!
Anyway sijui kwa nini ulipata division III wakati unataka kuchukua sayansi.Hujasema uko wapi lakini MASOMO YA online waajiri wengi hawatambui sifa hiyo hata upate PHD.Kuna vyuo vya masomo ya jioni kwa nini usisome huko hiyo kazi ambayo huna muda kabisa ni ipi hiyo? Kama uko Dar es salaam the best place kusoma jioni ni UNIVERCITY OF DAR ES SALAAM COMPUTING CENTRE (UCC) wana tawi chuo kikuu pale,POSTA mpya na maeneo mengine.Ila sasa ukienda usome kwa bidii IT ni fani inayobadilika mara kwa mara kutokana na maendeleo yake kwenda kasi sana kwa hiyo ukiingia huko uwe tayari kujiendeleza kusoma mara kwa mara.Yale uliyosoma mwaka huu usishangae mwakani ukienda na cheti chako kwa mwajiri mwingine akakwambia ujuacho ni outdated.Lakini kama lengo lako ni kusoma tu upate chetii/DIPLOMA usiendelee kusoma tena nakushauri tafuta fani ingine siyo IT.
nashuru sana mkuu kwa ushauri wako,nimeufurahia sana,ubarikiweUkitaka cheti nenda UCC, ukitaka kujua nenda kwenye hivi vyuo vya WAHINDI (Learn IT, New Horizon, CATS n.k). Suala la vyeti kutambulika ni ufukunyuku wa serikali yetu na ndio maana hatuendelei. Haya matatizo unayoyaona tiGO mtandao mara uko hivi mara vile ni matunda ya vyeti.
Huyo anayekwambia hbr za wewe kuwa na Div III hilo halimo. Division 5 ndio haina mashiko na kamwe usikatishwe tamaa na stupid academic rubbish. Go vocational dear boy na ukitaka kujua kuwa hao wanaojifanya wana high marks si kitu, angalia jinsi walivyoajiriwa kwa wingi na Bakhressa ambaye sidhani kama yeye ndio msomi saaaaaana. Go for skills, sio vyeti.