Nahitaji kujua hili kuhusu kusajiri jina la biashara.

MaMals

Member
Joined
Oct 31, 2013
Posts
46
Reaction score
7
Nina wazo langu la biashara ambalo lipo katika hatua za awali kabisa ambapo itachukua mpaka miezi 4 kukaa sawa. Sasa nafikiria kusajiri jina la biashara ili iwe mwanzo tu kulifanyia kazi wazo langu. Kwa sasa naona haina ulazima wa kuwa na ofisi na sihitaji kujisajiri katika mamlaka za kodi na zingine kama zipo. Naomba kujua kama inawezekana, nisije nikajisajiri ndo wakaanza kuniletea mambo za kodi wakati sijaanza kugenerate pesa. Wasalaam.
 
Kusajiri jina la biashara na kuanza kudaiwa kodi ni vitu viwili tofaoti.
 
Unaweza ukajisajili tu, ila kuhusu kodi na vingine utalipa utakapo anza kufanya biashara
 
Kuna njia mbili kuu za kusajiri biashara:-
1. Nenda Brela ukiwa na taarifa husika, watakupa fomu na kuijaza kisha kuwarudishia. Baada ya siku chache utasijiriwa jina la biashara yako. Utalipia kiasi kidogo sana cha fedha. TAHADHARI: Epuka Vishoka.
2. Tembelea Website yao (www.brela.go.tz) amabyo mbali na kupata taarifa husika za usajiri wa jina, lakini pia unaweza kujisajiri online.
3. Unaweza kuni Pm kwa msaada zaidi.
4. Kuhusu taarifa za Kodi tembelea www.tra.go.tz.
 
Appreciate that mkuu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…