Wanajamvi nahitaji msaada wa kufahamu historia ya mji wa Bagamoyo kaburi la Sharifa, kaburi la wapendanao, kaburi la Ally bwana juma, kisima cha ajabu, msikiti wa Bagamoyo, jengo la makumbusho na historia ya mamba wa Bagamoyo kiundani zaidi.
Nitashukuru mkinisaidia wanajamvi.
Wanajamvi nahitaji msaada wa kufahamu historia ya mji wa Bagamoyo kaburi la Sharifa, kaburi la wapendanao, kaburi la Ally bwana juma, kisima cha ajabu, msikiti wa Bagamoyo, jengo la makumbusho na historia ya mamba wa Bagamoyo kiundani zaidi.
Nitashukuru mkinisaidia wanajamvi.
Sio kaburi LA maiff ni "sharifa"NITAKUSAIDIA.
Baada ya mimi na wanafunzi wangu kwenda Bagamoyo tar30Aug.2014 nilijifunza haya;
1.KABURI LA MAIFU
=>Ieleweke kuwa lile si kaburi la Shariff bali la Maiff(mwanamke mwenye karama kama Shariff)
nisamehewe ikiwa nimekosea jina Maiff
=>Mjini Kaole(1200s) maji yote yalikuwa ya chumvi.
Watu walisumbuka kuchimba visima na kote walipata maji chumvi.
Msichana huyo alifanya dua,
akapewa maono na kuwaambia watu,
"Kwa uwezo wa Allah chimbeni hapa na hakika yatatoka maji matamu"
Kweli yalitoka maji safi,
wakajenga msikiti kando yake na vyote vipo hata leo.
¡èMaji kisimani hayapungui hata mchoteje,
hayaongezeki hata mvua inyeshe vipi¡è
=>Inaaminiwa watu wakiingia mle kaburin wakaomba hufanikiwa
Kanungila...HISTORIA YA MJI WA BAGAMOYO.
Bagamoyo ni jina kubwa sana hapa Tanzania kutokana na kujipatia umaarufu wake kufuatia vitu mbalimbali vilivyopo wilayani humo.
Mji huu wa bagamoyo upo mkoani pwani,iko kati miji ya kale na ya kihistoria kabisa ya waswahili katika nchi ya Tanzania,na ipo mwambao wa Bahari ya Hindi.
Katika mji huu kuna makumbusho mbalimbali ya kale kama maghofu,misikiti,minyororo ya kufungia watumwa,mbuyu mkubwa kuliko yote na kisima cha maji yanayotumika kunywa kuoga na kazi nyingine.
Wakazi wengi katika mji huo wa bagamoyo ni makabila mchanganyiko ya kibantu,kabila kubwa ni Wazaramo,lakini kuna makabila mengine kama wakwere,wazigua,na wadowe wote wakiishi katika mji huo ambao una vivutio vingi sana na vya kupendeza.
MAANA YA JINA BAGAMOYO.
Jina hili la bagamoyo lina maana kuwa hapo zamani lilikuwa linaitwa"Bwagamoyo" kutokana na hapo zamani kulikuwa na biashara ya utumwa kule Zanzibar ikifanywa na masultani kutoka Maskati Oman,ambapo watumwa walipokuwa wanaletwa bwagamoyo kwa ajili ya kusafirishwa kwenda zanzibar lazima wapumzike wakifika bwagamoyo,wanafurahi,wanacheza,wanakula na ndipo likaja jina la bwagamoyo wako na sio bagamoyo kama linavyoitwa sasa hivi.
NaaaamKanungila...
Mimi nitagusa hapo kwenye "utumwa kule Zanzibar ikifanywa na masultani kutoka Maskati Oman."
Soma historia ya utumwa ndiyo utakuwa katika hali ya kuelewa somo hili vyema.
Nakushauri uanze na "Transatlantic Slave Trade."