HISTORIA YA MJI WA BAGAMOYO.
Bagamoyo ni jina kubwa sana hapa Tanzania kutokana na kujipatia umaarufu wake kufuatia vitu mbalimbali vilivyopo wilayani humo.
Mji huu wa bagamoyo upo mkoani pwani,iko kati miji ya kale na ya kihistoria kabisa ya waswahili katika nchi ya Tanzania,na ipo mwambao wa Bahari ya Hindi.
Katika mji huu kuna makumbusho mbalimbali ya kale kama maghofu,misikiti,minyororo ya kufungia watumwa,mbuyu mkubwa kuliko yote na kisima cha maji yanayotumika kunywa kuoga na kazi nyingine.
Wakazi wengi katika mji huo wa bagamoyo ni makabila mchanganyiko ya kibantu,kabila kubwa ni Wazaramo,lakini kuna makabila mengine kama wakwere,wazigua,na wadowe wote wakiishi katika mji huo ambao una vivutio vingi sana na vya kupendeza.
MAANA YA JINA BAGAMOYO.
Jina hili la bagamoyo lina maana kuwa hapo zamani lilikuwa linaitwa"Bwagamoyo" kutokana na hapo zamani kulikuwa na biashara ya utumwa kule Zanzibar ikifanywa na masultani kutoka Maskati Oman,ambapo watumwa walipokuwa wanaletwa bwagamoyo kwa ajili ya kusafirishwa kwenda zanzibar lazima wapumzike wakifika bwagamoyo,wanafurahi,wanacheza,wanakula na ndipo likaja jina la bwagamoyo wako na sio bagamoyo kama linavyoitwa sasa hivi.