Nahitaji kujua juu ya biashara kukoboa na kusaga nafaka (mahindi)

Duniatunapita man

Senior Member
Joined
May 5, 2024
Posts
181
Reaction score
252
Habari wadau,. Kama mada inavyojieleza, nahitaji kupata uelewa wa biashara ya kukoboa na Kusaga mahindi. Ninapenda kuwa na mashine kwaajili hiyo Ili niweze kudunduliza kipato (mashine ya kutumia umeme).

Ni usagaji wa rejareja tu mtaani. Nahitaji kufahamu bei za mashine mpya na used. Gharama za uendeshaji K.V kodi za TRA, umeme, service n.k.

Pia vyanzo vya hasara na faida yake,. Eneo ni mkoani (Songea).
 
Habari wadau,. Kama mada inavyojieleza, nahitaji kupata uelewa wa biashara ya kukoboa na Kusaga mahindi. Ninapenda kuwa na mashine kwaajili hiyo Ili niweze kudunduliza kipato. Ni usagaji wa rejareja tu mtaani. Nahitaji kufahamu bei za mashine mpya na used. Gharama za uendeshaji K.V kodi za TRA, umeme, service n.k,. Pia vyanzo vya hasara na faida yake,. Eneo ni mkoani (Songea).
Nenda Sido,Lakini ushauri mwingine ni kusaga na kusindika unga itafaa zaidi,utakuja kunishukuru
 
Mkoa wa Ruvuma
Ok,mimi nimefanya hiyo biashara, huu ndio mchango wangu:

1.Kufanikiwa kwa biashara kunategemea na uwepo wa mahindi wa watu wa eneo unalofanyia biashara.

2.Sido wana bei sana,kama utapata fundi mzuri wa mtaani akutengenezee vinu vyote viwili (kusaga na kukoboa) hutajutia.

3.Unaweza kutumia mota moja kwa vinu vyote viwili(hapa iwe kuanzia 25hp) au ukanunua ya kukoboa kuanzia 15hp na kusaga 20hp.

4.Mota agiza dar au nunua huko huko ingawa dar ni bei chini kidogo.

4.Kuhusu faida:Mashine ni moja ya biashara zisizo na stresi na faida kubwa sana ukipatia eneo.

Uliza nikujibu kile ninachokijua.
 
Nenda Sido,Lakini ushauri mwingine ni kusaga na kusindika unga itafaa zaidi,utakuja kunishukuru
Kusindika uwe na mtaji mkubwa ili uione faida yake.Yaani uwe na mitaji mitaji miwili au mitatu.Maana unqsambqza kwa mqli kauli, unga unauzwa na baada ya aiku kadhaa wewe unapewa hela yako.Ila malighafi hawakopeshi unatakiwa kulipa cash pqmoja na usafiri.otherwise kwa dar faida inapatikana kwa kuuza pumba baada ya kukoboa.

Hesabu zake ni za hovyo sana.ukiona mtu yuko bize anasindika unga ujue hesabu yake ni kali sana.ukikurupuka na kamtaji kako ka kuungaunga utafunga biashara kwa kukimbia madeni.otherwise kama kamtaji kako ni ka mawazo fungua ya kukoba na kusaga kwa ajili ya watu wengine hapo utaokota okota.Na inabidi ukae mwenyewe golini
 
Hz ngoma used ni ngumu kuzipata maana ni biashara isiyo kuwa na mapicha picha,hvyo kupata mtu anaiuza ni ngumu

diesel engine mpya ni kama 1,300,000,used mpaka za laki 5 zipo,kinu chake kwa mafundi wa mtaani ni laki 6-7

Motor hp 20 bei 1,400,000 kinu chake laki 8_9

Ukiweka umeme wa elfu 10(unit 28) unaweza pata mpaka elfu 40-50 mauzo faida inaweza kuwa 30,000 kwa siku

Diesel engine sina uzoefu nayo

Kuna mafundi wanauza hz mashine zikiwa complete na bei inaweza kuwa 3 mil(yaan unauziwa kinu na motor na reli na mikanda ya mashine
images-2.jpeg
 
Umeshafeli tayari

Mikoa mizuri kwa biashara hiyo ni majiji makubwa kama Dar
Inategemea mkuu,kama anataka kwaajili ya biashara ya unga,unachosema kina ukweli kwa kiasi flani lakini kama kwa ajili ya biashara ya kuwagia wananchi,ruvuma atatoboa maana wananchi wana mahindi ya kutosha.Mimi moja ya mashine ipo mkoa wanaozalisha sana mahindi na biashara ni nzuri.
 
Amesema auze na rejareja haitamlipa
 
Ok,mimi nimefanya hiyo biashara, huu ndio mchango wangu:

1.Kufanikiwa kwa biashara kunategemea na uwepo wa mahindi wa watu wa eneo unalofanyia biashara.

2.Sido wana bei sana,kama utapata fundi mzuri wa mtaani akutengenezee vinu vyote viwili (kusaga na kukoboa) hutajutia.

3.Unaweza kutumia mota moja kwa vinu vyote viwili(hapa iwe kuanzia 25hp) au ukanunua ya kukoboa kuanzia 15hp na kusaga 20hp.

4.Mota agiza dar au nunua huko huko ingawa dar ni bei chini kidogo.

4.Kuhusu faida:Mashine ni moja ya biashara zisizo na stresi na faida kubwa sana ukipatia eneo.

Uliza nikujibu kile ninachokijua.
Bei ya 15hp, 20hp na hiyo 25hp Kwa dar es salaam inaweza kua kiasi gani!?
 
Umeshafeli tayari

Mikoa mizuri kwa biashara hiyo ni majiji makubwa kama Dar
Usimkatishe tamaa, Ruvuma inalisha unga wa mahindi mikoa ya mtwara na lindi, japokuwa wanaofnaya hizo biashara wana mitaji mikubwa.
 
Back
Top Bottom