Nahitaji kujua juu ya biashara kukoboa na kusaga nafaka (mahindi)

Habarii, biashara ya mashine imegawanyika,sehem mbili,

Kuwasagia watu mizigo yao ambayo wao wanakuja nayo wewe unasaga na kuchukua pesa,

Au

Unasaga mahindi na kuuza sembe,

Kama unataka kusaga vipeto vya wateja ninakushauli nunua mashine namba 75 hii ni rafiki sana upate mota hp kuanzia 16 na kuendelea , mota iwe na rpm kuanzia 1200,

Kama mtaji wako mdogo nunua mota hp 30 hii itakufanya utumie mot moja kwa vinu vyote viwili yaani unaweza kusaga na kukoboa kwa mara moja, ,

Unaweza nunua mashine ya kukoboa rola 3 japo kwa sasa rola 3 ni rafiki zaid,



Kama unataka kununua mashine ya kusaga sembe kwa,aliji ya kuuza ninakushauli ununue mashine ya kusaga namba 100, upate mota hp 40 na kuendele iwe na rpm kuanzi 1200

Unatakiwa kuapata na mashine ya kusaga ya rola 3 au 4,


Kwnn ninakwambia rpm kuanzia 1200?


Mzunguko halisi wa mashine kuanianzia rpm 1300 mpk 1400 sasa ukiwa na mota chini ya rpm 1000 ili upate mzunguko huu lzma uweke pull kubwa ambayo itakuwa mzigo kwa mota, mfano jamaa alikuwa na mota ya hp 50 lkn rpm yake ilikuwa 900 aliweka puli ya nch 18 ambayo ilikuwa na uzito zaid ya kilo 10, hii ni mgizo mkubwa sana kwa mota kwa maana kabla haijaanza kufanya kazi inakuwa ishabeba mzigo tayali,


Ukiwa na mota yenye rpm 1300 unaweza weka pull nch 6 au 5 ambayo itakuwa na uzito wa kilo 4 au 6,

Swala la pili kqma unahitaji kusaga sembe ya kuuza kwa vile upo songea itakulazima uchue mahindi ya huko huko, lkn mahindi bora ni kutoka kilosa , dodoma na tanga, lkn kwa vile upo huko itabidi utafute mahindi ya huko huko,


Mashine usinunue sido, tafuta fundi wa mtaani anaweza kutengeneza au ukakuta ishatengenezwa ukanunua tu, moto unaweza kununua hata used , mota bora ni kampuni ya ABB ukikosa nunua siemensi ukikosa nunua hizi za kichina za sasa, ,

Mashine ya kusaga sembe za kuuza kila kitu kiwa na mota yake kwa usalama zaid ,

Lkn hii itakufanya ufanye kazi kubwa kwa muda mfupi na usalama wa mikanda ,

Ile toa weka ya mikand itafanya mikanda iishe haraka sana,
Kama unataka kusaga semve kuuza anza kwa uchache ,

Ikiwa mtaji wako mdogo nenda kwenye mashine za watu usage sembe ukauze hii itakufanya usiwe na gharama kubwa sana, tumia mifuko ilioandikwa super sembe hii haina mmiliki inauzwa tu, usitumie nembo ya mtu au mfuko wa mtu bila ridhaa na ikibidi kimaandisihi,

Kusaga swmbe kwenye mashine ya mtu kwako itakuwa bora hasa kipindi unaanza kwa sababu, hautakuwa na sehemu nyingi za kulipa lkn pia kama soko utakuwa haulielewi unaweza kutoka ktk biashara hii na ukiwa hauna cha kupteza,


Kama unahitaji mengine mengi karibu m p, hapa hapawezi tosha
 
Ushauri mujarabu kabisa kwa mtoa mada.
 
Asante, kwasasa target ni kusaga kwaajili ya wateja wa mtaani ambao watakuja na mahindi yao.
 
Na
omba namba yako bosi
 
Shukrani kwa mchanganuo,,,

Mpk kukamilisha gharama zote zinachezea kiasi gani?
 
Tusaidie mchanganuo Sasa mkuu ambao hatujaanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…